CLOUDS MEDIA GROUP YATANGAZWA KUWA MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI MWAKA 2017
HomeJamii

CLOUDS MEDIA GROUP YATANGAZWA KUWA MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI MWAKA 2017

Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi tuzo Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi ...

SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
KONGAMANO LA TANZANIA YA VIWANDA LAFANA MKOANI IRINGA
MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA RC MSTAAFU ABBAS KANDORO



Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi tuzo Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa  Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon leo Jumamosi Septemba 16,2017 mkoani Tanga (Habari/Picha na Oscar Assenga na Kadama Malunde)


Jopo la Majaji Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 limeitangaza Clouds Media Group kuwa mshindi wa Tuzo hiyo kwa mwaka 2017. 

Tuzo hiyo imetolewa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC wakati wa mkutano wake mkuu wa unaofanyika katika ukumbi wa Tanga Beach Resort mkoani Tanga. 

Tuzo hiyo imekabidhiwa  kwa uongozi wa Clouds Media Group na Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura. 

Mbali na kupewa tuzo hiyo,pia Clouds fm imekabidhiwa hundi ya shilingi milioni 10 kama pole kwa changamoto waliyopitia baada ya kituo cha matangazo kuvamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda aliyekuwa ameambatana na askari polisi. 

Mwenyekiti wa Jopo la Majaji Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017,Jenerali Ulimwengu alisema madhumuni ya tuzo ya mwangosi ni kumuenzi na kumkumbuka kwa kumpa mwanahabari au chombo cha habari tuzo yenye jina lake. 

“Jopo la majaji mwaka huu tunaitangaza Clouds Fm kuwa mshindi wa tuzo ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa sababu tarehe 17,Machi,2017 wanahabari wa Clouds walivamiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam akiwa na askari polisi akiwataka kutangaza habari ambayo hawakuitaka lakini wafanyakazi hao wakakataa kutangaza habari hiyo,huu ni ushujaa kwani hawakukubali kutii amri ambazo zilikuwa kinyume na kazi waliyofundishwa na uandishi wa habari”,alisema Ulimwengu. 

“Lengo la tuzo hii iliyoanzishwa mwaka 2013 na UTPC ni kupinga vitendo viovu wanavyofanyiwa waandishi wa habari , hutolewa kwa mwandishi wa habari anayefanya kazi nchini aliyekutana na madhila katika utendaji kazi wake ama chombo cha habari ambacho kimekutana na madhila”,alieleza Ulimwengu. 

Aliongeza kuwa tuzo hiyo inalenga kuwafanya wadau wa habari ikiwemo serikali kutambua kazi ya waandishi wa habari. 

“Daudi Mwangosi alikuwa mwenyekiti Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa,aliuawa Tarehe 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo mkoani humo,akitekeleza majukumu yake,ni mwandishi wa habari wa kwanza nchini Tanzania kuuawa akiwa kazini, kifo chake kilishtua na kusikitisha watu wengi duniani”,alieleza.
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi tuzo Tuzo ya Uandishi wa Kishujaa na Ulitukuka ya Daudi Mwangosi mwaka 2017 kwa  Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon
Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura cheti cha ushindi kwa  Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon

Mkurugenzi wa Tanzania Media Foundation,Ernest Sungura akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa  Afisa Mahusiano kutoka Clouds Media Group Simalenga Simon.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CLOUDS MEDIA GROUP YATANGAZWA KUWA MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI MWAKA 2017
CLOUDS MEDIA GROUP YATANGAZWA KUWA MSHINDI WA TUZO YA DAUDI MWANGOSI MWAKA 2017
https://4.bp.blogspot.com/-plo7tWTyz_w/WbzaPQSwgUI/AAAAAAAAR1A/asz7lDW-XcAFREoVZtBu9Yq-75vF5_yqQCLcBGAs/s640/1.jpg
https://4.bp.blogspot.com/-plo7tWTyz_w/WbzaPQSwgUI/AAAAAAAAR1A/asz7lDW-XcAFREoVZtBu9Yq-75vF5_yqQCLcBGAs/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/clouds-media-group-yatangazwa-kuwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/clouds-media-group-yatangazwa-kuwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy