BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA MBALIMBALI
HomeJamii

BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA MBALIMBALI

Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali...

MAPAMBANO YA DAWA ZA KULEVYA NA UVUVI HARAMU YASHIKA KASI WILAYANI NYAMAGANA
MAKAMU WA RAIS AONGOZA WATANZANIA KUAGA MIILI YA WANAFUNZI WALIOPATA AJALI MKOANI ARUSHA
TUME YA HAKI ZA BINADAMU YATOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA MSIBA MZITO MKOA WA ARUSHA


Na Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017.

Akiwasilisha Bungeni Muswada huo leo Mjini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa lengo la marekebisho yaliyopendekezwa ni kuboresha utekelezaji wa Sheria hizo kwa kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia sheria hizo na kuongeza masharti mengine ili kuleta uwiano kati ya Sheria zilizorekebishwa na sheria zilizopo.

"Muswada wa Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa mwaka 2017 unapendekeza kufanya marekebisho katika sheria 11 na kufuta sheria moja" amefafanua Mwanasheria Mkuu wa Serikali. 

Aidha, Masaju amesema kuwa masuala muhimu yaliyozingatiwa katika Muswada huo ni pamoja na kubadilisha vifungu vya Sheria kwa kufuta baadhi ya vifungu vya sheria hizo na kuviandika upya, kufuta baadhi ya maneno kwenye vifungu vya sheria, kuzingatia maneno mapya, kuongeza vifungu vipya na kufuta sheria moja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Mohamed Mchengerwa amesema kuwa Kamati inashauri Serikali kuhakikisha Kamati maalumu ya kumshauri Waziri kuhusu misamaha ya kodi iundwe na wataalamu waliobobea kutoka katika fani na maeneo tofauti tofauti ili kujenga uwezo wa kamati hiyo katika kumshauri Waziri husika kuhusu misamaha hiyo ya kodi.

Nae Ally Saleh Ally kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Katiba na Sheria amesema kuwa kambi hiyo inashauri kuwa haitoshi kuifuta RUBADA pekee bali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamiko ya wananchi wanaoituhumu kupora ardhi na hatua stahiki kwa wote waliohusika zichukuliwe.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA MBALIMBALI
BUNGE LAPITISHA MUSWADA WA MABADILIKO YA SHERIA MBALIMBALI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEib4QPbK0TrzHFSSkUM2zvuSX2E-vYcn-Sd-FWRNyw4hp2qu7oOrT3uT_M8R58uSLaptL1xuw0eEKkctgT14Smm31L8jE8pvrVjRTf3nAO6kCXOlUs7j4RVdJcMvwM9tI6aX9dyQKrWbM4D/s400/images.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEib4QPbK0TrzHFSSkUM2zvuSX2E-vYcn-Sd-FWRNyw4hp2qu7oOrT3uT_M8R58uSLaptL1xuw0eEKkctgT14Smm31L8jE8pvrVjRTf3nAO6kCXOlUs7j4RVdJcMvwM9tI6aX9dyQKrWbM4D/s72-c/images.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/bunge-lapitisha-muswada-wa-mabadiliko.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/bunge-lapitisha-muswada-wa-mabadiliko.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy