AZAKI ZA ZANZIBAR ZAWEZESHWA NA FCS KUFANYA MAFUNZO YA KWA VITENDO MOROGORO
HomeJamii

AZAKI ZA ZANZIBAR ZAWEZESHWA NA FCS KUFANYA MAFUNZO YA KWA VITENDO MOROGORO

 Washiriki wa mafunzo kutoka Asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutawanyika kila kundi kuele...

WAZIRI JENISTA MHAGAMA AFUNGUA MKUTANO WA WADAU KUJADILI NAMNA BORA ZAIDI YA UTEKELEZAJI WA SHERIA YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI
KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
BALOZI WA TANZANIA NCHINI SRI LANKA, MHE.BARAKA LUVANDA AWASILISHA HATI ZAKE ZA UTAMBULISHO

 Washiriki wa mafunzo kutoka Asasi za Kiraia za Visiwani Zanzibar, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutawanyika kila kundi kuelekea katika vijiji viwili tofauti vya Msowelo na Matombo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.  
 Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao.

  Kundi lililokuwa likielekea Msowelo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
  Kundi lililokuwa likielekea Matombo likipiga picha ya pamoja mbele ya gari lao
 Wakiwasili Msowelo
Asasi za Kiraia kutoka Zanzibar zimeendelea na mafunzo ya
siku mbili kuhusu Utetezi na Ushawishi wa Sera mkoani Morogoro. Asasi
mbalimbali kutoka Zanzibar na Pemba ziko katika ziara ya Mafunzo iliyoratibiwa
na Foundation for Civil Society (FCS) chini ya mwamvuli wa Association of Non
Governmental Organizations of Zanzibar (ANGOZA) inakutanisha wawakilishi Zaidi
ya 40 kutoka Zanzibar ambao wamekuja kujifunza namna mashirika ya MVIWATA
(Muungano wa Vikundi vya Wakulima Wadogo Tanzania) na MPLC (Morogoro Para-Legal
Center).
Katika siku ya pili washiriki hawa wamepata fursa ya kwenda
uwandani ili kukutana na wanufaika wa kazi mbalimbali zinazofanywa na MVIWATA
na MPLC. MVIWATA imewapeleka washiriki wilayani Kilosa katika kijiji cha
Msowelo ambapo kijijini hapa kumekuwa na migogoro ya Wkulima na Wfugaji ambapo
kijijini hapa MVIWATA imefanikiwa kutumia mtandao wake wa msingi kupaza sauti
kwa serikali ili kutenga maeneo ya wakulima. Tayari wilayani hapa kuna mashamba
9, ambayo yamefutwa na yamekabidhiwa katika mamlaka ya wilaya ili yagawiwe kwa
wananchi.
Kwa upande wa MPLC yenyewe inawaonesha washiriki hawa kazi
zao katika eneo la Matombo ambako huko pia MPLC inafanya kazi za utetezi wa
haki za umiliki wa ardhi kwa makundi mbalimbali yanayokabiliwa na changamoto
hiyo. Shirika hilo limejizolea sifa kwa kazi zake mkoani Morogoro na pia ni
shirika kongwe ambalo linafanya kazi za utetezi na ushawishi mkoani Morogoro.
Washiriki kutoka Zanzibar wanatumia nafasi hii kubaini
changamoto mbalimbali zinazoyakumba makundi mbalimbali katika jamii ilhali
kukiwa na mapungufu katika sera na maamuzi hali inahyowahitaji wananchi kufanya
ushawishi na utetezi wa haki za kila kundi ili kuchochea jamii kubaki ikiishi
kwa mani na ikiendesha maisha kwa mafanikio.
 Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Zainab Kisegele, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
 Mwenyekiti wa Mtandao wa Msingi Msowelo, Ally Omary, akizungumza na wanaasasi za Kiraia kutoka Visiwa vya Zanzibar,wakati walipofika kijijini hapo Msowelo kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kujifunza namna ya kupambana na changamoto za migogolo ya Ardhi na njia wanazoweza kutumia kutatua migogolo katika Kata za Vijiji.
 Washiri wakisikiliza kwa umakini
 Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Msowelo
 Washiriki waliokuwa wakielekea Matombo wakiwa katika gari kuelekea katika mafunzo kwa vitendo.
 Wakiwa katika mafunzo
 Wakiuliza maswali kwa wenyeji wao ili kujifunza zaidi
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
 Mafunzo yakiendelea Matombo.....
Ushuhuda .......
Picha ya pamoja baada ya mafunzo kwa walioelekea Kijiji cha Matombo.
 Baada ya mafunzo kwa pande zote mbili Msowelo na Matombo, washiriki walikutana tena na kuungana kwa majadiliano baada ya mafunzo kwa vitendo
 
Washiriki wakijielezea jinsi walivyoweza kujifunza kutoka kwa wenzao walokokwenda.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AZAKI ZA ZANZIBAR ZAWEZESHWA NA FCS KUFANYA MAFUNZO YA KWA VITENDO MOROGORO
AZAKI ZA ZANZIBAR ZAWEZESHWA NA FCS KUFANYA MAFUNZO YA KWA VITENDO MOROGORO
https://i.ytimg.com/vi/7muHDtJM_Ho/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/7muHDtJM_Ho/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/azaki-za-zanzibar-zawezeshwa-na-fcs.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/azaki-za-zanzibar-zawezeshwa-na-fcs.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy