Leo Jumatatu Agosti 21,2017, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack (aliyesimama pichani) amefanya mkutano wa hadhara katika viwan...
Leo Jumatatu Agosti 21,2017, Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack (aliyesimama pichani) amefanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Zimamoto karibu na soko la Nguzo Nane Mjini Shinyanga kusikiliza kero za wananchi.
Mkuu huyo wa mkoa wa Shinyanga aliyekuwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa,na watumishi mbalimbali wa serikali alisikiliza kisha kujibu kero za wananchi huku pia akitoa nafasi kwa watumishi kutoka idara mbalimbali kujibu hoja na kero za wananchi.
Miongoni mwa kero zilizoibuka eneo la mkutano huo ni pamoja na ardhi ambapo baadhi ya wananchi walieleza kutoridhishwa namna ardhi inavyotolewa na jinsi migogoro ya ardhi inavyotatuliwa.
Kero nyingine ni ukosefu wa maadili kwa baadhi ya askari polisi waliodaiwa kutowajali wananchi wanaofika katika kituo cha polisi huku askari polisi wakiendelea kufanya mambo yao ikiwemo kuchat kwenye mitandao ya kijamii badala ya kuhudumia wananchi wanaofika kituoni.
Suala la vumbi katika barabara ambazo ujenzi wake haukamiliki mjini Shinyanga nalo likiibuka kwamba afya zao ziko hatarini kutokana na vumbi hilo.
Pia wananchi wakaomba kuwekewa taa za barabarani pamoja na askari wa usalama barabarani katika eneo la Japanese Corner mjini Shinyanga ambapo panadaiwa kutokea ajali za mara kwa mara.
Kero ya bei kubwa ya maji nayo haikusahaulika,wananchi walieleza kuwa bei ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA).
Hali kadhalika wananchi wakaomba kuwekewa sehemu ya kupumzikia walau wawekewe mwamvuli katika mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga.
Wananchi pia waliomba kuongezwa kwa waganga katika kituo cha afya Kambarage ambacho kinadaiwa kuzidiwa na idadi ya wagonjwa wanaofika kupata huduma.
Wazee nao wakatoa kilio chao cha kutaka huduma bora ya afya wakiomba kuingizwa kwenye bima ya afya badala ya kupewa tu dawa bure.
Akijibu hoja mbalimbali za wananchi,Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack aliwataka watumishi wa umma kuzingatia maadili yao ya kazi katika kuwatumikia wananchi huku akiwasisitiza kutatua kero za wananchi kwa wakati.
Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa pale inapotokea mkandarasi anayejenga barabara mjini hajamwaga maji kwenye barabara kwani wamemwagiza kuwa anamwaga maji ili kuepusha vumbi.
Aidha baada kusikiliza kero za wananchi,mkuu huyo wa mkoa aliagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyokubaliana wakati wa mkutano huowa hadhara ifikapo Septemba 15,2017 ili kuhakikisha kero za wananchi zinapungua.
Aidha baada kusikiliza kero za wananchi,mkuu huyo wa mkoa aliagiza kupewa taarifa ya utekelezaji wa mambo mbalimbali waliyokubaliana wakati wa mkutano huowa hadhara ifikapo Septemba 15,2017 ili kuhakikisha kero za wananchi zinapungua.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara kusikiliza kero za wananchi leo mjini Shinyanga-Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akizungumza
Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mkutano,kushoto ni Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akifuatiwa na kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule na mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga
Mkazi wa Shinyanga mjini Ndyamkama Venant akieleza kero zake kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Mkutano unaendelea,viongozi wakiandika dondoo muhimu/maswali ya wananchi
Mwananchi akieleza kero zake
Mkazi wa Shinyanga akieleza kero yake
Mwananchi akieleza kero yake
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akisikiliza kero za wananchi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akijibu kero za wananchi kuhusu jeshi la polisi
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,Simon Haule akizungumza
Afisa Ardhi wa manispaa ya Shinyanga,Alex Rutailwa akijibu hoja za wananchi kuhusu migogoro ya ardhi.
Viongozi mbalimbali wakiwa eneo la mkutano
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),Injinia Sylivester Mahole akijibu hoja za wananchi kuhusu maji.
Mkutano unaendelea
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akijibu hoja za wananchi
Mkutano unaendelea
Mwananchi akieleza kero zake
Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela akijibu hoja za wananchi
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mwananchi akiuliza swali wakati wa mkutano huo
Mkutano unaendelea
Wananchi wakiwa katika mkutano huo
Mwananchi akieleza kero yake
Mwananchi akieleza kero yake
Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Dk. Rashid Mfaume akijibu hoja za wananchi
Mkazi wa Shinyanga Mjini,Mohammed Diwani Mkambala akieleza kero yake kwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Wananchi wakiwa katika foleni wakiuliza maswali na kueleza kero zao
Mwananchi akieleza kero yake.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
COMMENTS