MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE, (UCSAF), NA MAKAMPUNI YA SIMU WASAINI MKATABA WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SITA WA KUPELEKA MAWASILIANO KWA WOTE
HomeJamii

MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE, (UCSAF), NA MAKAMPUNI YA SIMU WASAINI MKATABA WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SITA WA KUPELEKA MAWASILIANO KWA WOTE

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati), akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko w...

WAZIRI MKUU ATEMBELEA KIWANDA CHA KUUNGA MATREKTA YA URSUS
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA VIWANDA CHINA NA MABALOZI
PROF. MBARAWA AITAKA BODI YA DMI KUBORESHA MIUNDOMBINU

Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati), akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu
(CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Bw.
Le Van Dai (kulia) wakati wakisaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya simu kwa kujenga miundombinu maeneo ya vijijini, chini ya Mradi wa sita wa kufikisha
mawasiliano kwa wote, kwenye makao makuu ya UCSAF barabara ya Bagamoyo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2017. UCSAF imesaini makubaliano kama hayo na makampuni mengine ya simu hapa nchini ikiwemo, Vodacom Tanzania PLC,
Airtel, tigo na TTCL.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Mawasiliano Kwa Wote Nchini,
(UCSAF), umesaini mkataba na makampuni matano ya simu hapa nchini wa utekelezaji wa Mradi wa Sita wa Kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Manyaa
Mbarawa. 
Makampuni yaliyotia saini
mkataba huo ambao utayawezesha, kujenga miundombinu ya kupeperusha mawasiliano ya simu kwenye mmbalimbali hususan vijijini ni pamoja naHalotel, Airtel, Vodacom Tanzania PLC, TTCL na TIGO.
Waziri Profesa Mbarawa alishuhudia Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF kwa niaba ya Mfuko, akisaini mikataba hiyo na Maafisa Watendaji Wakuu wa makampuni hayo mbele ya waandishi wa habari.


Kwa mujibu wa maafisa wa UCASAF, kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza malengo makuu ya Mfuko ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya
mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu.
Lakini pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano
hafifu. 
Malengo mengine ni pamoja na
Kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo
ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;
Kutengeneza mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la
kiushindani;
Maafisa hao wamesema lengo linguine ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei
nafuu.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amewahakikishia wawekezaji ushirikiano uklio dhahiri kutoka serikalini na kuwataka, waongeze kasi ya uboreshaji wa mawasliano ya simu ili wananchi
hususan wa vijijiniwaweze kutumia teknolojia ya mawasiliano kuharakisha maendeleo yao.




 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akitoa hotuba yake,

Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola, akizungumza kwabla ya kumkaribisha Profesa Mbarawa kutoa hotuba,

 Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Ulanga, akielezea
lengo la kusainiwa kwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa Mradiwa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote.


 Baadhi ya wawakilishi wa makampuni ya simu,

 Bi. Beatrice Singano Mallya kutoka Airtel, akifurahia hotuba.

 Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF,

 Afisa kutoka kampuni ya Halotel,

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa
kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCSAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017

Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Mallya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa
wote.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati) akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao, wakibadilishana hati baada ya
kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini.


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati) akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Simon Karikari, wakisaini mkataba huo


Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Simon Karikari, wakibadilishana hati baada ya
kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.


 Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Mhandisi Cecil Nkomola Francis, wakisaini
mkataba huo


 Mhandisi Ulanga, akimpongeza Bw. Ferrao wa Vodacom
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Simon Karikari, akiwa miongoni mwa maafisa wenzake wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri
 Profesa Mbarawa, akipena mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya
UCSAF, Joseph Kilongola.
 Wakuu wa makampuni ya simu za
mikononi nchini.
 Bw. Ferrao, akitoa hotuba ya
shukrani kwa niaba ya wenzake
 Profesa Mbarawa na Mhandisi Ulanga, wakionyeshana kitu
 Profesa Mbarawa akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Joseph Kilongola,
 Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF,
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE, (UCSAF), NA MAKAMPUNI YA SIMU WASAINI MKATABA WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SITA WA KUPELEKA MAWASILIANO KWA WOTE
MFUKO WA MAWASILIANO KWA WOTE, (UCSAF), NA MAKAMPUNI YA SIMU WASAINI MKATABA WA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA SITA WA KUPELEKA MAWASILIANO KWA WOTE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_LJfyrOK4RAI3mdnb2SJeKCdNNGYviDNnWlNoNekA-HhyU2u-v6u9ub8nXZmjCOF6oRcf3LIH2PFl8xqg7dcbJVTamkd75SpZwA-GHUx_PJWoNZFxvtonw-24_syFKgUPDjrOzdYRrOgB/s640/5R5A2983.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_LJfyrOK4RAI3mdnb2SJeKCdNNGYviDNnWlNoNekA-HhyU2u-v6u9ub8nXZmjCOF6oRcf3LIH2PFl8xqg7dcbJVTamkd75SpZwA-GHUx_PJWoNZFxvtonw-24_syFKgUPDjrOzdYRrOgB/s72-c/5R5A2983.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mfuko-wa-mawasiliano-kwa-wote-ucsaf-na.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/mfuko-wa-mawasiliano-kwa-wote-ucsaf-na.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy