Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya...

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana
na Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National
Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya
China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei
23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza
na Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National
Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National.
Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa tayari
kumsindikiza na Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China
National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National
Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akimkaribisha Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin
aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo na Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin
aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
![]() |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
akimsindikiza Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin
aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
|
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki
Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu jijini
Dar es Salaam Mei, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza
na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu
jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
![]() |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza baada ya mazungumzo Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na
Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei aliyemtembelea Ikulu
jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika
mazungumzo na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei
aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam Mei 23, 2017
(PICHA NA IKULU)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425 |
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Shirikisho la Taifa la Utengenezaji wa Mitambo ya Viwanda la China (China National Machinery Industry Federation - CNMIF) kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itawapa ushirikiano wa kutosha katika mpango wao wa kuwekeza katika uzalishaji wa nishati ya umeme, viwanda na kilimo hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo tarehe 23 Mei, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa CNMIF na Mbunge wa Bunge la Wananchi wa China Bw. Zhan Xin.
Mhe. Dkt. Magufuli amesema Tanzania imejiwekea malengo ya kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka Megawatts kati ya 1,500 na 1,800 zinazozalishwa hivi sasa hadi kufikia Megawatts 10,000 na kwamba ili kufikia malengo hayo wawekezaji wanakaribishwa kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vilivyopo kama vile gesi, makaa ya mawe na jua.
“Kwa hiyo Ndg. Zhang Xin kawaambie wawekezaji wenzako wa China waje Tanzania, nchini zetu ni ndugu na marafiki wa miaka mingi, itakuwa jambo jema wakija kuunga mkono juhudi zetu za kujenga viwanda kwa kuzalisha umeme mwingi na pia kushiriki katika miradi mingine ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na Balozi wa Ufaransa hapa nchini Mhe. Malika Berak ambapo viongozi hao wamezungumzia utekelezaji wa mambo mbalimbali ya ushirikiano pamoja na miradi ya maendeleo iliyotokana na makubaliano ya Mkutano wa wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa uliofanyika hivi karibuni.
Viongozi wengine ambao leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli ni Kaimu Balozi wa Uturuki hapa nchini Bw. Yunus Belet na Kaimu Balozi wa Jamhuri ya Korea Bw. Songwon Shin.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
23 Mei, 2017
COMMENTS