Na Mwandishi Wetu. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Baloz...
Na Mwandishi Wetu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uholanzi nchini
Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika Ikulu kwa lengo la kuaga baada ya
kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini.
Makamu wa Rais alimhakikishia Balozi huyo kuwa Tanzania itazidi
kuimarisha uhusiano wake na nchi ya Uholanzi hasa katika sekta ya kilimo,
elimu na uboreshwaji wa mazingira ya uwekezaji
ili kufikia lengo la Tanzania ya Viwanda.
Aidha, Mhe.Balozi aliahidi kuwa mjumbe mzuri wa Tanzania na
atarejea mara kwa mara kuja kutembea kwani Tanzania ina watu wema na vivutio
vingi vya utalii.
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia hapa nchini umemalizika. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya kitabu kiitwacho 'The Netherlands at its best’ kutoka kwa Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaam kuaga rasmi kwani muda wake wa kutumikia hapa nchini umemalizika. |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam |
 |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jaap Frederiks na Kaimu Balozi Lianne Houben (kulia) mara baada ya mazungumzo yaliofanyika Ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) |
COMMENTS