Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kon...
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Salum Maulid Salum, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kongamano la nne la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje litakalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. Hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Mkurugenzi wa PPR Pascal Mayalla akiuliza swali katika mkutano na waandishi wa habari uliozungumzia Kongamano la kitaifa la Watanzania wanaoishi nje uliofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Uratibu wa Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi Bi. Adila Hilali Vuai akijibu masuali yaliyoulizwa na wandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kongamano la kitafa litalofanyika tarehe 23 na 24 Agosti hapa Zanzibar. (kushoto) Muandishi wa habari Rahma Suleiman wa Chuchu Fm Redio. (Picha na Makame Mshenga)
Mwanahabari na mtangazaji gwiji Paskali Mayalla sio mwana Diaspora, lakini ni mmoja wa wadau ambaye amewahi kuishi nje ya nchi kwa muda ' Mimi Paskali Mayala nimewahi kuishi nje kwa muda mfupi mfupi katika nchi mbalimbali, na nimewahi kufanya kazi tena sio kubeba box, bali kubeba zege ndani ya jiji la London, hivyo nina mwanga kidogo kuhusu diaspora, ila kwenye hili naomba Watanzania tushikamane na kutoa maoni yetu ili tuijenge nchi yetu' anasema mwanahabari huyo. Hima tujitoe kila mmoja wetu na tukubali kuwa jukumu ni letu sote na tunao wajibu wa kutimiza katika maendeleo ya nchi yetu.
Hivyo basi bodi ya Diaspora inawaomba wadau wote ushirikiano kwenye kongamano hili, kwa kuhudhuria moja kwa moja au kwa njia ya 'proxy', ili kutoa mawazo yenu Tanzania iwasaidiaje ili kukuwezesha kila mmoja kuisaidia nchi yetu.
Tanzania itajengwa na Watanzania wote wakiwemo wana diaspora. Kitu cha kwanza ni kuomba ushiriki wako physically kwa wale wenye nafasi wanaweza kujisajili kupitia ukurasa hapo chini DIASPORA: Home Page
Kwa wale ambao hawatapata nafasi ya kuwepo physically, wanaweza kushiriki by proxy, kwa vile dunia sasa ni kijiji kimoja, wanaweza kushiriki by proxy.
Ufunguzi rami wa Kongamano lenyewe litatangazwa live za TV za Tanzania. Pia tutatangaza live kupitia video streaming kwenye youtube hivyo wana diaspora wote wenye nafasi wanaweza kufuatilia kupitia youtube, facebook, tweeter na mitandao ya kijamii.
Tunatarajia kupata ushirikiano wako tujadiliane namna bora ya kuapata maoni na mawazo ya watu mbalimbali ili Tanzania isonge mbele kwa wana wana Diaspora wote.
Uzalendo sio kujiuliza "Tanzania Ikusaidie nini, bali ni wewe kujiuliza je nimeisaidia nini nchi yangu Tanzania?". Kwa vile wana diaspora wengi wako nchi za nje na wamepata bahati ya kupata exposure kubwa, tunahitahitaji mawazo yenu, ili tuweze kuisaidia nchi yetu Tanzania ingare na kupiga hatua mbele katika maendeleo.
COMMENTS