NA K-VIS BLOG KAMANDA mpya wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Lazaro Mambosasa, ameanza kazi leoAgosti 29, 2017 kwa kuitisha mku...

NA K-VIS BLOG
KAMANDA mpya wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP, Lazaro Mambosasa, ameanza kazi leoAgosti 29, 2017 kwa kuitisha mkutano na waandishi wa habari kwa kujitambulisha na kisha kuonana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mhe. Paul Makonda.(pichani juu)
Kamanda Mambosasa ambaye ameteuliwa kuliongoza jiji kiusalama akitokea mkoani Dodoma, amesema yeye siyo mgeni na jiji na kwamba aliwahi kufanya kazi kama Kamanda wa Polisi Jamii Tanzania. “Nilifanya kazi hiyo kuunganisha ushirikishwaji wa jamii na polisi katika swala zima la ulinzi na usalama.” Alisema.
Lakini pia alisema kabla ya hapo alikuwa OCD Kimara kabla ya kupandishwa cheo na kuwa msaidizi wa RPC Ilala, (Staff One).



COMMENTS