DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI
HomeJamii

DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la...

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA WATUMISHI WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
WAZIRI MKUU AKABIDHI KADI ZA MATIBABU KWA WAZEE 280
WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA VIONGOZI KUJADILI MASUALA YA JESHI LA MAGEREZA








NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
NAIBU
Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa
ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko
Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dkt.
Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara
kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na
eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko
Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Hakikisheni
mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni,
chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara
waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi
wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.
Akiwa
kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam,
Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo
cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.
Ongezeko
la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji
mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya
wakazi wa maeneo hayo.
“Naomba
niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu,
mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni
wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa
Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa
Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie
wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika.”
Alisema.
Dkt.
Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa
maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili
kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme
wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka,
aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri
yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam


 Msaidizi
wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid
James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt.
Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo
cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam
 Dkt. Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kurasini.




Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es
Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (watatu kushoto), akimpatia maelezo ya
maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto)

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwa na  Msaidizi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid
James, (kushoto), akiongea na waandishi wa habari.










Meneja wa TANESCO Mkoa wa
Temeke, Mhandisi Jahulula akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani


 Meneja wa TANESCO Mkoa
wa
Temeke, Mhandisi Jahulula, (wapili kulia), akifafanua baadhi ya mambo kwenye eneo ambalo
patajengwa kituo cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji, Kigamboni
jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Nishati na
Madini, Dkt. Medard Kalemani(katikati).
 Fundi wa TANESCO akiwa kazini pale Kigamboni.
 Mhandisi Jahulula, (kushoto), akionyesha mahala mpaka wa eneo hilo la mradi unapoishia.
 Dkt. Kalemani (katikati), na viongozi wa TANESCO wakiwa kwenye eneo hilo la Kimbiji



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI
DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheyuvTDKRaz0Q7YRwjwCiBcvpQMtVb0xaftihg7FnC_8tr1dXr5GRpYqD67mCa7hj0DSwgyAWucDdhBJq8TOuAPAtj0rYs3BGj40qM7CBoxBEDzgOv6TrEdRbkHOlpLPeP_j86Rouz4O9d/s640/5R5A4197.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEheyuvTDKRaz0Q7YRwjwCiBcvpQMtVb0xaftihg7FnC_8tr1dXr5GRpYqD67mCa7hj0DSwgyAWucDdhBJq8TOuAPAtj0rYs3BGj40qM7CBoxBEDzgOv6TrEdRbkHOlpLPeP_j86Rouz4O9d/s72-c/5R5A4197.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dkt-kalemani-aitaka-tanesco-kuunganisha.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dkt-kalemani-aitaka-tanesco-kuunganisha.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy