DKT. KALEMANI AENDELEA KUZINDUA MIRADI YA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (REA PHASE III MIKOA YA KUSINI NA RUKWA
HomeMikoani

DKT. KALEMANI AENDELEA KUZINDUA MIRADI YA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (REA PHASE III MIKOA YA KUSINI NA RUKWA

Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akiwasili eneo la uzinduzi Mkoani Rukwa, akiwa amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu ...




Naibu Waziri Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akiwasili eneo la uzinduzi Mkoani Rukwa, akiwa amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mheshimiwa Saidi Mtanda.

Na Henry Kilasila - Rukwa


Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameendelea na ziara za uzinduzi wa Miradi
ya Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA PHASE III) ambapo Agosti 14, 2017 alikuwa Mikoani
Rukwa katika Kijiji cha Kabwe Wilaya ya Nkasi.



Dkt. Kalemani alisema jumla ya Shilingi Bilioni 42.5 zitatumika kupeleka umeme
katika Mkoa huo na kuongeza Mradi huo utatekelezwa katika vipindi viwili
tofauti ambapo sehemu ya kwanza itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 111.



"Sehemu ya pili itahusisha vijiji 145 ambapo itaanza baada ya
kukamilika  kwa sehemu ya kwanza. Kufikia mwaka 2021 vijiji vyote vya Mkoa
wa Rukwa vitakuwa vimepatiwa umeme".Alisema Dk. Kalemani.



Aidha, Dkt. Kalemani alimtambulisha Mkandarasi atakayejenga Mradi wa REA
Mikoani humo Kampuni ya Kitanzania ya Nakuroi Investment Company Limited.

Alimwagiza Mkandarasi kuhakikisha anapeleka umeme Kijiji kwa Kijiji na
Kitongoji kwa Kitongoji bila kuruka na sehemu zinazotoa huduma za Kijamii kama
Mashule, Zahanati, Magereza, Visima vya maji, Nyumba za Ibada na sehemu
mbalimbali.

Pia alitoa maagizo kwa TANESCO kupeleka Ofisi katika Kijiji cha Kabwe na katika
maeneo yote yenye Wateja wengi lakini wapo mbali na Huduma za TANESCO.

Aliongeza kwa kuwataka Mameneja  na Watalaamu wa TANESCO kutokukaa Ofisini
bali wawafuate Wateja.

Awali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCo, Dkt. Tito E. Mwinuka aliwaomba
Wananchi hao wa Kabwe kuwa waaminifu na kutoa ushirikiano kwa Watendaji wa
TANESCO kabla na hata baada ya Mradi kukamilika.

"Muitunze miundombinu ya umeme, msiihujum wala kuichoma moto".
Alisema Dkt. Mwinuka.

Alisema TANESCO imejipanga kuhakikisha Wananchi hao wanapata huduma ya umeme
iliyobora na ya uhakika.

 Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy  aliwaeleza Wananchi kuwa mradi huo wa
usambazaji umeme vijijini hauna malipo ya fidia hivyo watoe ushirikiano kwa
wakandarasi hao wakati wanatekeleza mradi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Nkansi Mheshimiwa Saidi Mtanda aliushukuru Uongozi wa TANESCO
kwa kwani umekuwa ukitoa ushirikiano pale unapohitajika.

"Mheshimiwa Mgeni Rasmi katika Kijiji cha Nyamare kwenye chanzo cha maji
tulileta Mkandarasi akatukadilia bei ya Transifoma milioni 60, tuliwasiliana na
uongozi wa TANESCO wametufungia Transfoma kwa pesa zao milioni 24".
Alisema Mheshimiwa Mtanda.

Mheshimiwa
Naibu Waziri wa
Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani alimalizia uzinduzi Mkoani Rukwa kwa kuwakabidhi Wazee kumi zawadi ya kifaa cha UMETA.



 Naibu waziri Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani akifurahia baada
ya kuzindua mradi wa REA RUKWA

Kutoka kushoto Mkurugenzi Mkuu REA, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
Dkt. TITO E. Mwinuka katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa Kampuni ya
Nakuro
Investment Company Limited inayojenga Mradi huo wa umeme Mkoani humo.
Naibu waziri Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dkt Medard Kalemani akipata maelezo ya namna kifaa cha UMETA kinavyofanya kazi kutoka kwa Bw. Lucas Kusare Afisa Huduma kwa Wateja Mkoa wa Rukwa



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. KALEMANI AENDELEA KUZINDUA MIRADI YA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (REA PHASE III MIKOA YA KUSINI NA RUKWA
DKT. KALEMANI AENDELEA KUZINDUA MIRADI YA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU (REA PHASE III MIKOA YA KUSINI NA RUKWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjf96AxFSK1hPNR4ldY2wIkPo4fsr7QrfDIAc8yqsglEfY0FZsMCf365n4TGsChl0GpAJHiIiWPwYisCHoxy3YlWE4o8gEC0Py0lT0Nk0YyzuUaxXYfOjHzyL5VkyX5GTRIKLiQNEx2wBOP/s640/pic1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjf96AxFSK1hPNR4ldY2wIkPo4fsr7QrfDIAc8yqsglEfY0FZsMCf365n4TGsChl0GpAJHiIiWPwYisCHoxy3YlWE4o8gEC0Py0lT0Nk0YyzuUaxXYfOjHzyL5VkyX5GTRIKLiQNEx2wBOP/s72-c/pic1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dkt-kalemani-aendelea-kuzindua-miradi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/dkt-kalemani-aendelea-kuzindua-miradi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy