· Yasajili wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha miezi mitatu · Wateja wapya 1.038 milioni wa Airtel Money wasajiliwa...
· Yasajili wateja wapya 132,826 kwa kipindi cha
miezi mitatu
· Wateja wapya 1.038 milioni wa Airtel Money
wasajiliwa
![]() |
| Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya akiongelea mafanikio kya Airtel baada ya na jinsi Airtel ilivyojipanga kutoa huduma bora zaidi. |
Airtel Tanzania ndio kampuni ya simu za mkononi nchini Tanzania
ambayo imefanikiwa kuongeza wateja wengi kwenye robo ya pili ya mwaka huu huku
makampuni ya simu za mkononi wakishindania kuongeza wateja wapya na watumiaji
wa huduma za kifedha kulingana na ripoti ya Tanzania Communications Regulatory
Authority (TCRA).
Kulingana na ripoti ya robo ya pili ya 2017 (TRCA’s Quarterly
Communication Statistics Report), makampuni ya simu za mkononi Tanzania
yaliongeza watumiaji wapya wa huduma za kifedha 1,059,163 milioni kwa kipindi
cha April mpaka Juni.
Kutokana na idadi hiyo, Airtel Tanzania ilisajili wateja wapya
1,038,193. Hii inamaanisha ya kwamba kwa kipindi hicho asilimia 98 ya wateja wa
huduma za kifedha za simu za mkononi wapya waliojiunga na Airtel Tanzania.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kuhusu
mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano
alisema ‘Hii ni ishara nzuri kuwa Airtel inatoa suluhisho sahihi kwa huduma za
kifedha kwa makampuni ya simu za mkononi hapa Tanzania. Kwa mfano tuangalie
huduma ya mikopo rahisi ya Timiza inayotolewa kupitia Airtel Money, hatimaye imeanza
kuzaa matunda’.
Huduma ya mikopo ya Timiza inadhihirisha juhudi zetu za kutoa
suluhisho inapokuja suala ya huduma za kifedha kwa kutumia simu za mkononi. Pia
inaenda samba samba na juhudi za serikali za kuhakikisha kuwa wafanya biashara
wadogowadogo na wakati wanapata huduma ya mikopo yenye marshati nafuu, alisema
Singano.
Ikiwa na ongezeko la 1.038 milioni, Airtel Tanzania kwa sasa ina
jumla ya wateja milioni 5.9 wa Airtel Money kwenye soko ambalo jumla ya
makampuni matano ya simu za mkononi yanashindania wateja milioni 20. Airtel
Tanzania pia imefanikiwa kusajili laini mpya 132,826 kwenye robo ya pili ya
mwaka na hivyo kufikisha jumla ya watejakuwa milioni 10.3. Kwa ujumla, jumla ya
wateja wapya wa simu za mkononi waliongeza na kufikia 40.358 milioni mwishoni
mwa mwezi Juni kutoka 39.856 mwishoni mwa Machi mwaka huu.
Kwa kuendeleza uwekezaji zaidi nchini kwa mujibu wa Singano
anathibitisha kuwa Airtel Tanzania inazidi kukua vizuri huku kampuni hiyo ikiendelea
kuwekeza zaidi kwenye miradi mbali mbali ili kufuta wateja wengi wapya.
Moja ya mradi mkubwa wa
uwekezaji ni mradi wa U900. Kulingana na Singano, Mradi wa U900 unatafuta
kuboresha miundombinu ya kiufundi kwa nia ya kuongeza kiasi cha data na
kuboresha kasi ya data
"Hii mikakati yetu ya kuimarisha
maisha ya Tanzania kupitia huduma za kidigitali. Katika jiji la Dar es
Salaam zaidi ya maeneo 300 tayari yamebadilishwa, mpango wetu ni kueneza mradi
wetu wa U900 kwa mikoa ya Mwanza, Morogoro, Dodoma, Arusha na kisha katika
masoko mengine yenye uwezo mkubwa hapa nchini Tanzania, "aliongeza
Singano.


COMMENTS