Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya uwekeji wa jiwe la msingi la u...
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza leo jijini Dar es
Salaam katika hafla ya uwekeji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la
kisasa la huduma za dharura Hospitali ya Temeke ambalo ujenzi wake
utagharimu zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa
Japan Nchini Tanzania.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akikata utepe kwa kushirikia na
Mkuu wa Wilaya wa Temeke,Felix Lyaniva pamoja Mwakilishi wa Balozi wa
Japani Nchini,Hiroyuki Kubota,kwenye hafla
fupi ya uwekeji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la
huduma za dharura Hospitali ya Temeke, ambalo ujenzi wake utagharimu
zaidi ya shilingi Million 800 linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini
Tanzania.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akipongezana na Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini Tanzania,Hiroyuki Kubota.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na viongozi wa halmashauri ya
manispaa ya temeke wakikagua ujenzi wa jengo la huduma za dharura.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa halmashauri ya manispaa ya temeke na watumishi wa Hospitali
hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda leo ameweka jiwe la
msingi la ujenzi wa jengo la kisasa la huduma za dharura Hospitali ya
Temeke ambalo ujenzi wake utagharimu zaidi ya shilingi Million 800
linalofadhiliwa na ubalozi wa Japan Nchini Tanzania.
Akizungumza
wakati wa hafla hiyo Mheshimiwa Makonda amesema jengo hilo litakuwa na
uwezo wa kusaidia zaidi ya watu 2,000 kwa siku ambapo litakuwa na chumba
cha upasuaji,chumba cha ICU,vyumba vya uangalizi maalumu wa wagonjwa
pamoja na vyumba vya madaktari.
Aidha
jengo hilo litakuwa na vyumba maalumu vya watoto (njiti) akinamama na
wababa ambapo lengo ni kuhakikisha mgonjwa yoyote wa dharura iwe wa
ajali,upasuaji kwa kinamama wajawaziito,malaria ya ghafla,moto na
wanaobanwa na kifua wanapatiwa huduma ya haraka ambapo kwa hatua hiyo
itasaidia kupunguza mlundikano wa wagonjwa wa dharura Hospital ya Taifa
Muhimbili kama Rais Dkt.Magufuli anavyotaka.
“Mimi
nimeshuhudia watu wengi wakipoteza maisha kwa kukosa huduma za dharura,
hii ndio iliyonisukuma kutafuta kila njia ili wananchi wangu wasipoteze
maisha kwasababu tu ya kukosa hutuma ya haraka, nikaamua kumtafuta
balozi wa Japani na kumshirikisha jambao hili, Balozi aliponisikiliza na
kunielewa akakubali kuniunga mkono katika mapambano yangu ya kuboresha
huduma za afya kwa wananchi hasa wanyonge na ameshanipa fedha kwaajili
ya ujenzi wa jengo hilo na hivi tunavyoongea tayari mkandarasi ameanza
na ujenzi” Alisema Makonda.
Aidha
Mheshimiwa Makonda amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo utachukuwa miezi
sita hadi kukamilika na kueleza kuwa dhamira yake ni kuhakikisha Dar es
salaam inakuwa mkoa unaotoa huduma bora za Afya.
“Watu
hatukumbukwi kwa maneno bali kazi tulizofanya, kwa kuwa Rais Magufuli
amenipa Mkoa niongoze na mimi ni lazima nitumie akili na kipaji ambacho
Mungu amenipa kutatua Changamoto za Afya katika Mkoa wangu”, Alisisitiza
Makonda.
Kwa
upande Mwakilishi wa Balozi wa Japani Nchini Tanzania Bwana Hiroyuki
Kubota amesema serikali ya Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania
katika masuala mbalimbali huku mkuu wa wilaya ya Temeke Mheshimiwa Felix
Lyaniva akimpongeza Makonda kwa namna anavyopambana kutatua kero za
wananchi

COMMENTS