RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO

Mhe. David Kafulila Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza ...


Mhe. David Kafulila
Na Editha Karlo- Globu ya Jamii Kigoma

RAIS Wa Jamuhuri wa Muungano Wa Tanzania Dkt John Magufuli amempongeza aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini ,David Kafulila kwa kujitoa Muhanga kutetea Watanzania kupitia sakata la Escrow(IPTL) na kuonesha uzalendo Mkubwa ambao hawezi kusahaulika katika historia ya Tanzania.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Nguruka, leo Katika uzinduzi wa Mradi mkubwa wa Maji uliopo Tarafa ya Nguruka katika Wilayani Uvinza, alisema atakuwa mnafiki akishindwa kumpongeza Kafulila kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuibua Ubadhilifu uliofanywa na Kampuni ya IPTL ambapo kwasasa suala hilo ameanza kulifanyia kazi na mafanikio yameanza kuonekana.

Amesema Kafulila alitukanwa sana alipo ibua sakata la Escrow na kuitwa majina mengi ya kudhalilishwa kama tumbili na mengine mengi ya ajabu kwasababu ya uzalendo wake wa kutetea Taifa.

"Mimi ninafahamu unapoibua kitu cha kizalendo lazima usemwe, hivyo ninampongeza Kafulila kwa uzalendo wake kwa nchi na nitaendelea kumpongeza maisha yangu yote"alisema Magufuli.Magufuli alisema maendeleo hayana chama ndio maana Kafulila alijitoa kwa hali ya juu na kutetea fedha za Wananchi zilizo kuwa zikiibiwa na mafisadi wachache na kujinufaisha wao.

"Ninajua Kafulila ulitukanwa sana wakati wa kuibua sakata la Escrow, wapo watu walikuita tumbili mimi najua wewe sio tumbili ,matumbili ni wao wewe najua ni wa Chama kingine lakini umefanya kazi kubwa ya kulinda maslahi ya nchi, kwahiyo nitakuwa mnafiki sana nisipo kupongeza kitu ulichokifanya ni kikubwa Kwa,Taifa naomba nikupongeze kwa hilo",

Alisema Kiongozi mzuri ni yule ambae anatetea wananchi bila kujali chama wala siasa za uchochezi , hivyo atahakikisha kuwa Wananchi hawateseki na Wale ambao wameiba fedha za serikali na Wananchi wanazirudisha bila kujali nyadhifa walizonazo, ili pesa hizo zitumike katika kuleta maendeleo.

Rais Magufuli aliwaahidi Wananchi wa Nguruka atahakikisha anatatua kero ya Maji na umeme katika kata yao,kuhusu suala la umeme atamtuma Waziri wa Nishati na madini ili aweze kutatua tatizo hilo na kuwasaidia Wananchi kuepukana na shida hizo.

Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kigoma kwa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa Maji mkubwa katika kata ya Nguruka uliogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 ambao unatarajiwa kukamilika desemba 30 mwaka huu ambao utafuta kero ya maji kwa wananchi wa kata ya Nguruka.

Akiongea kwa njia ya simu na mtandao huu akiwa jijini Dar es Salaam aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kigoma kusini kupitia tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi David Kafulila kuhusu kauli ya Rais Kafulila amesema kuwa Rais amekuwa akimtia moyo kwani anaona kazi aliyokuwa akiifabya sasa imeanza kuleta matokeo mazuri.

"Kwakweli nafarijika na inanipa moyo wa kizalendo zaidi ninapo ona Rais anaunga mkono sakata la Escrow ambalo mimi ndo nililiibua wakati nikiwa mbunge japo nilipitia kwenye kipindi kigumu "alisema Kafulila

Kafulila alisema kuwa wakati akiwa mbunge kwenye sakata la Escrow msimamo wake na Rais ulikuwa unafanana toka bungeni.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
RAIS DKT MAGUFULI AMFAGILIA KAFULILA NYUMBANI KWAO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3_-hvsyUdzydDSPArensTynOmdVCU3jMHBDxVbmxFNgv_6HovOJzIj28A_opjTIYd41gK5Oll_97rNCTfhuXkW7JZnqq3I8RES6J0x_XoHiVb5WBkaxZNH0krtBnqTszV5-2Uc8aw9ys/s320/kafulila.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3_-hvsyUdzydDSPArensTynOmdVCU3jMHBDxVbmxFNgv_6HovOJzIj28A_opjTIYd41gK5Oll_97rNCTfhuXkW7JZnqq3I8RES6J0x_XoHiVb5WBkaxZNH0krtBnqTszV5-2Uc8aw9ys/s72-c/kafulila.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/rais-dkt-magufuli-amfagilia-kafulila.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/rais-dkt-magufuli-amfagilia-kafulila.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy