MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI
HomeJamii

MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI

Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii ul...

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU DAR ES SALAAM LEO
JARIDA LA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 159
RED CROSS YAKABIDHI KADI ZA UANACHAMA IDARA YA MAAFA

Mtandao mpya unaoundwa na Radio na vyombo vya habari vya kijamii Tanzania chini ya shirika la vyombo vya habari vya maudhui ya kijamii uliosajiliwa kwa jina la TANZANIA  DEVELOPMENT INFORMATION ORGANIZATION-TADIO umeanzishwa rasmi baada ya kuvunjika kwa mtandao wa zamani wa COMNETA.
Tukio hilo limetokea Julai 28, 2017 katika mkutano mkuu wa kwanza ambao pamoja na mambo mengine ulichagua safu mpya ya viongozi wa mtandao huo.  Shirika la mtandao wa vyombo vya habari jamii Tanzania uliokuwa na jina la COMMUNITY MEDIA NETWORK OF TANZANIA – COMNETA, limevunjika rasmi mwezi machi mwaka huu.
Katika mkutano huo kuwa kuundwa kwa shirika hilo jipya kunalenga kuhakikisha kunakuwa na mtandao makini wa Radio na vyombo vingine vilivyojikita katika kuibua kwa kuandika na kutangaza masuala ya kijamii kwa ajili ya maendeleo.
Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe wakati wa mkutano huo.
Akihutubia katika mkutano huu kaimu mkuu wa ofisi ya UNESCO Tanzania, ambao ni wafadhili wakubwa wa mtandao huo  Bw. Christophe Legay kwa niaba ya Mkuu wa ofisi Bi. Zulmira Rodrigues amepongeza hatua iliyofikiwa na Radio wanachama ya kuunda mtandao mpya.
Alieleza kuwa UNESCO itaendelea  kufanya kazi bega kwa bega na shirika hilo jipya la TADIO ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma sahihi za kihabari zitakazosaidia kuboresha maisha yao na kuchochea maendeleo ya upashanaji wa habari nchini.
Bw. Christophe amehimiza kwamba vyombo vya jamii vinao wajibu mkubwa wa kuhakikisha sauti za watu wanaowahudumia hasa wanaoishi vijijini.
Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize akizungumza jambo na wajumbe mara baada ya uchaguzi. Katikati ni mmoja wa wajumbe wa bodi ya TADIO, Maimuna Msangi na Katibu Mtendaji wa TADIO, Marco Mipawa.
Aliwaasa kushughulika na masuala ya kibinadamu na si watu binafsi.
Wakati huo huo Mtandao huo unaoundwa na jumla ya Radio 32 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar, umefanya uchaguzi mkuu na kuwapata viongozi watakaosimamia shughuli zake kwa miaka mitatu ijayo.
Uchaguzi huo ulitanguliwa na tukio la kujiuzuru kwa viongozi wa mpito waliochaguliwa mwezi Machi mwaka huu, baada ya kutangazwa rasmi kuvunjika kwa muungano wa awali wa radio jamii wa COMNETA.
Katibu Mtendaji mpya wa TADIO, Marco Mipawa (kulia) akizungumza jambo mara baada ya uchaguzi kufanyika. Kutoka kushoto ni Balozi Mstaafu Mh. Christopher Liundi, Mkuu wa idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania, Christophe Legay, Mwenyekiti mpya waTADIO Bw. Prosper Kwigize na Mjumbe wa Bodi ya TADIO, Maimuna Msangi.
Akitangaza matokeo, msimamizi wa uchaguzi huo ambae pia ni mlezi wa ushirika huo, Balozi mstaafu Mheshimiwa Christopher  Liundi, alimtangaza  Bw. Prosper Kwigize aliyekuwa mgombea pekee kuwa  Mwenyekiti  mpya  baada ya kupata kura  za ndiyo  26  kati ya kura   30 zilizopigwa  na  wajumbe  waliohudhuria.
Balozi  Liundi, pia alimtangaza  Bw. Marco Mipawa kuwa Katibu Mtendaji baada ya kupata kura   28  za ndiyo, Aidha Mipawa pia alikuwa mgombea pekee katika uchaguzi huo.
Viongozi  wengine waliochaguliwa ni pamoja  na Mweka Hezina, Shaaban Ali Makame aliepata kura  24  za ndiyo. Pia mkutano huo uliwachagua wajumbe  sita wa Bodi  ya  shirika hilo la TADIO ambao ni Maimuna Msangi kutoka Pangani FM, Gladys Mapeka kutoka Radio Kilosa, Ali  Mbarouk Omar kutoka kutoka Klabu ya Waandishi wa Habari wa Pemba (PPC),  Ali Khamis kutoka Adhana FM Zanzibar, John Baptist kutoka Dodoma FM na  Anthony Masai kutoka Triple A FM.
Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi (kulia) akimpongeza akimpongeza Mwenyekiti mpya wa TADIO, Prosper Kwigize.
Akizungumza  baada ya kutangaza matokea hayo, Balozi Liundi aliitaka safu ya uongozi  mpya   kuongoza  kwa kufuata  katiba  na malengo ya  shirika hilo  kwa lengo la kutetea maslahi  mapana  ya wananchi kwa kupitia kazi  zinazofanywa na radio  za kijamii.
Kwa  upande  wake,  Mwenyekiti mpya wa TADIO Bw. Prosper Kwigize amewashukuru wajumbe kwa kuchagua safu mpya ya uongozi na kuahidi kujenga ushirikiano mpya ambao utawezesha kufikiwa kwa malengo ya kuanzishwa kwa mtandao huo wa ushirikiano wa vyombo vya habari vya kijamii.
Bw. Kwigize ametoa wito kwa wadau wengine hususani Radio za kitaifa, magazeti, waandishi wa habari za mitandaoni (bloggers) Muungano wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT, TAMWA, MISA, Baraza la Habari Tanzania, Runinga na Vilabu vya waandishi wa habari mikoani kushirikiana na shirika la TADIO ili kutoa huduma stahiki kwa jamii.
Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi akimpa pongezi Katibu wa TADIO Bw. Marco Mipawa (shati la kitenge) mara baada ya matokeo kutangazwa.
Amehimiza pia serikali na taasisi zake kutoa ushirikiano kwa TADIO ili misimamo, dira na malengo yanayoibuliwa na serikali yawafikie wananchi kwa haraka kupitia muungano huo wa Radio za mikoani.
Amesisitiza kuwa, mtandao huo wa TADIO una ofisi na studio ya kisasa ndani ya Chuo Kikuu Huria Tanzania – OUT makao makuu Kinondoni Dar es Salaam ambako kazi ya ofisi na studio hiyo ni kuratibu shughuli za mtandao pamoja na kuandaa vipindi ambavyo vitakuwa vikisambazwa kwa radio wanachama.
Aliitaka safu ya uongozi mpya  kuacha kufanya kazi kwa mazoea, kujenga umoja na  mshikamano  pamoja na  kufanya kazi kwa bidii  na ubunifu  ili kuyafikia malengo ya  ushirika huo.
Mtandao wa TADIO unafadhiliwa na UNESCO chini ya mradi wa SIDA/SDC.
Msimamizi wa uchaguzi huo mwanasheria Harold Sungusia (mwenye tai) akimpongeza Mwenyekiti mteule wa TADIO, Prosper Kwigize.
Picha ya pamoja ya viongozi wa TADIO, Balozi mstaafu Mh. Christopher Liundi na Msimamizi wa uchaguzi huo Mwanasheria Harold Sungusia.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI
MTANDAO MPYA WA VYOMBO VYA HABARI VYA KIJAMII WASAJILIWA NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEhK-cSKf-xyS2kSv1bQUkuA9s_JvyMtZNRjDHP3GcdPYwxIZT_3kCYUA5bNUXljOgtUDf1gGW5XCmIYO5L14vmGdWNnwSxHKqMMKEUdvOSCKruo2V7IjGq5jkC1uVPY88-qiZ9rP6mf4GSZ1Q5C1rP09rp07b4B_A1vdqxGB_f1Boaa=s0-d-e1-ft
https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEhK-cSKf-xyS2kSv1bQUkuA9s_JvyMtZNRjDHP3GcdPYwxIZT_3kCYUA5bNUXljOgtUDf1gGW5XCmIYO5L14vmGdWNnwSxHKqMMKEUdvOSCKruo2V7IjGq5jkC1uVPY88-qiZ9rP6mf4GSZ1Q5C1rP09rp07b4B_A1vdqxGB_f1Boaa=s72-c-d-e1-ft
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mtandao-mpya-wa-vyombo-vya-habari-vya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mtandao-mpya-wa-vyombo-vya-habari-vya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy