MPINA AWAPONGEZA VIONGOZI WA MIKOA WILAYA NA HALMASHAURI NCHINI WALIOTEKELEZA KIKAMILIFU AGIZO LA USIMAMIZI WA USAFI WA MAZINGIRA.

NA EVELYN MKOKOI –MASWA Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amewapongeza viongozi wa mikoa wilaya ...


NA EVELYN MKOKOI –MASWA

Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amewapongeza viongozi wa mikoa wilaya na halmashauri nchini waliotekeleza kwa kiwango cha kuridhisha agizo la kusimamia utekelezaji wa siku ya kitaifa ya kufanya usafi na kuhakikisha usafi wa mazingira katika maeneo yao unaimarishwa.

Mpina ameyasema hayo leo Wilayani Maswa alipokuwa akishiriki zoezi la kufanya usafi kitaifa na kuongeza kuwa majina ya viongozi hao pamoja na wale ambao wamezembea kutekeleza agizo hilo yatafikishwa kwa Mhe. Rais na Mhe. Makamu kwa hatua za kiutendaji.

“Hatuwezi kufikia mapinduzi ya uchumi wa viwanda kama taifa litaendelea kuwa chafu kwani tutaendelea kupoteza nguvu kazi nyingi kutokana na maradhi yanayosababishwa na uchafu, hivyo viongozi wa mikoa na wilaya wana jukumu kubwa la kusimamia usafi wa mazingira.” Alisisitiza Mpina.

Naibu Waziri Mpina aliongeza kwa kusema kuwa serikali imeona kuwa usafi ndio afya na usafi ndio maisha na ndio maana Serikali imeitenga siku ya Jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa ni siku maalum kwa ajili ya usafi wa Mazingira.

Akiwa ziarani wilayani Maswa Mhe. Mpina alibaini changamoto mbalimbali za kimazingira zinazoikumba wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo katika soko la Maswa, mazingira yasiyoridhisha ya kufanyia biashara sokoni na ukosefu wa maji katika machinjio ya wilaya, ambapo aliekeza uongozi wa Halmashauri kuhakikisha ndani ya miezi mitatu changamoto ya upungufu wa matundu ya choo iwe imefanyiwa kazi, kuwepo kwa mabanda ya kisasa ya kufanyia biashara katika soko hilo na kuhakikisha kunakuwepo na maji ya kutosha wakati wote katika machinjio.

Kwa Upande wake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Bw. Vivian Christopher, alieleza kuwa Halmashauri yake imetenga fedha kwa ajili ya kushughulikia changamoto hizo katika Bajeti wilaya kwa mwaka wa fedha 2017/2018.



Pichani Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Akizungumza na Baadhi ya wakazi wa Halmashauri ya Wilaya wa Maswa (hawapo katika picha) leo baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MPINA AWAPONGEZA VIONGOZI WA MIKOA WILAYA NA HALMASHAURI NCHINI WALIOTEKELEZA KIKAMILIFU AGIZO LA USIMAMIZI WA USAFI WA MAZINGIRA.
MPINA AWAPONGEZA VIONGOZI WA MIKOA WILAYA NA HALMASHAURI NCHINI WALIOTEKELEZA KIKAMILIFU AGIZO LA USIMAMIZI WA USAFI WA MAZINGIRA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAqSsQzMVG-hnJZvjtj9CP6BRS3lMzqssiUL8i98orGqE9COti98hx8EvhXu5Puf0j-EoQAO6fSHrigfz8i1z-wc4LTj6AVpR_uhKWc-_wzib982ADmTp9CCbQaMo83Ethcf7mEfAC6Cg/s640/DSC_0130.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgAqSsQzMVG-hnJZvjtj9CP6BRS3lMzqssiUL8i98orGqE9COti98hx8EvhXu5Puf0j-EoQAO6fSHrigfz8i1z-wc4LTj6AVpR_uhKWc-_wzib982ADmTp9CCbQaMo83Ethcf7mEfAC6Cg/s72-c/DSC_0130.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mpina-awapongeza-viongozi-wa-mikoa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/07/mpina-awapongeza-viongozi-wa-mikoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy