Watoto watano waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa vifaa maalum vya kusaidia kusikia (Cochlear ...
Zoezi hilo limefanywa leo na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaam kutoka MEDEL .
Daktari Bingwa wa magonjwa ya
Masikio, Pua na Koo Edwin Liyombo amesema Juni 5 na 6 mwaka huu
watoto hao walifanyiwa upasuaji huo kwa mara ya kwanza na kuwekewa vifaa
maalum kwa ajili ya kusikia (Internal complete) lakini leo wamekuja
kuwekewa na kuwashiwa vifaa vya nje(External complete) ili waweze
kusikia.
Kwa upande wake mtaalam wa vifaa
vya usikivu Fayaz Jaffer amesema baada ya kuwekewa kifaa hivyo watoto
hao wanapaswa kurudi kila baada ya wiki mbili kwa miezi mitatu na baada
ya hapo watarudi wiki mbili kwa miezi sita ili kufanyiwa mazoezi.
‘’Baada ya hapo wanaanza
kuwafanyia mazoezi ya kuongea ( speech therapy) ndani ya mwaka mmoja na
kadiri umri unavyozidi kwenda watakuwa wameshaanza kusikia na kujifunza
kuongea na kupelekwa kujifunza zaidi katika shule za kawaida na si shule
maalum kama ilivyozoeleka” amesema mtaalam huyo.
Juni 7 mwaka huu Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alizindua
huduma ya upasuaji wa kupandikizaji wa vifaa vya usikivu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili , ambapo katika Hospitali za Umma Tanzania
imekuwa nchi ya kwanza kutoa huduma hiyo na ya pili katika nchi za
Ukanda wa Afrika Mashariki ikitanguliwa na Kenya.
COMMENTS