Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyomb...
- Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh Shomari Mchongoma (kushoto) akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.
- Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola (kulia) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo akizungumza katika mkutano wa vyombo vya habari ulioandaliwa na kushirikisha viongozi wa dini kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kutoka kushoto ni Sheikh Shomari Mchongoma (BAKWATA), Bw. Lucas Singili (CCT), pamoja na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose.
- Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw. Lucas Singili (katikati) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT na Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Kulia ni Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose na Sheikh Shomari Mchongoma wa BAKWATA (kushoto).
VIONGOZI wa
Dini wamekemea vitendo vya ukatili kwa watoto na kwani vimekemewa hata
katika vitabu vya dini, huku wakimtaka kila mmoja kumlinda mtoto pamoja
na kueneza elimu ya malezi. Viongozi hao walioshiriki katika mkutano wa
vyombo vya habari ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake
(TAMWA) kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Jumuiya ya
Kikristo Tanzania (CCT) kwa pamoja waliungana na TAMWA kukemea vitendo
vya kikatili wanaofanyiwa watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku
ya Mtoto wa Afrika.
Akizungumza
Mwakilishi kutoka Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Sheikh
Shomari Mchongoma alisema jamii kwa pamoja inapaswa kuungana na kukemea
vitendo vya kikatili kwani ni kinyume cha imani zetu. Alisema jambo
pekee ambalo linaweza kufanikisha mapambano hayo ni jamii kumrudia
mwenyezi Mungu na kukemea vitendo viovu anavyochukizwa navyo.
"...Wakati
umefika tuangalie ni namna gani kumkomboa mtoto wetu kwenye wimbi la
mateso ya kikatili ambayo wamekuwa wakitendewa baadhi ya watoto wetu.
Mtoto anaweza kuwa salama endapo tutaungana na kukemea vitendo hivyo
bila kujali tofauti zetu," alisema Sheikh Mchongoma.
Kwa
upande wake, Mwakilishi kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Bw.
Lucas Singili alisema mtoto anaitaji malezi ya pamoja kwa ushirikiano
ikiwa ni kuwaweka karibu ili waweze kukua katika malezi mema. Watoto
hawapaswi kutengwa wala kufanyiwa vitendo vya kikatili zaidi ya kuwapa
msaada kutoka kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla ili waweze kuwa
raia wema wenye maadili katika taifa la baadaye.
- Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose (wa kwanza kulia) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA). Wengine kushoto ni viongozi wa dini.
- Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose (kulia) akizungumza katika mkutano wa pamoja na viongozi wa dini kutoka BAKWATA, CCT kukemea vitendo vya kikatili dhidi ya watoto, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika. Kulia ni Ofisa Miradi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Godfrida Jola akifuatilia mazungumzo hayo.
- Sehemu ya wanahabari na maofisa wa TAMWA wakiwa katika mkutano huo.
Aidha
aliongeza kuwa mtoto hapaswi kuchokozwa kwa nmna yoyote kama
wanavyofanyiwa ukatili na mambo yasio mema na baadhi ya watu.Alisema
hata vitabu vya dini vimekemea aina yoyote ya uchokozi dhidi ya watoto,
hivyo kuiomba jamii kushirikiana katika kutoa elimu ya malezi mema kwa
watoto waje kuwa raia wema na bora baadaye. "...Mtoto achokozwi,
usimchokoze mtoto hata maandiko ya dini yanasema hivyo...," alisisitiza
Bw. Singili wa CCT.
Naye
Mtaalamu wa Saikolojia ya Jamii, John Ambrose akizungumza na wanahabari
katika mkutano huo, alisema yapo madhara makubwa yanayomtokea mtoto
endapo akipitia katika vitendwa vya unyanyasaji. Alisema mtoto
anapokumbana na vitendo vya unyanyasaji anapoteza matumaini kwa jamii,
anapoteza imani, anajenga hofu na thamani yake inashuka hivyo kuishi
katika maisha mabaya zaidi.
Alieleza
kuwa, mtoto anayefanyiwa vitendo vya kikatili asipo badilishwa huenda
akawa mkatili zaidi hapo baadaye jambo ambalo tunaweza kujikuta
tunaandaa taifa hatari, hivyo kumtaka kila mmoja katika nafasi yake
kukemea vitendo vya kikatili dhidi yao ili kumlinda mtoto.
COMMENTS