Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC G...
Spika
wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia)akizungumza pale ugeni kutoka
Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES
ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Mwenyeji
na kiongozi wa Msafara Askofu Oscar John.
Spika
wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikat) akimsikiliza Mhe.William Ngeleja akizungumza wakati Umoja wa Wanamichezo wa Mpira wa
Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini kwake
Mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kulia) akimsikiliza Askofu Oscar John
(aliyesimama) akizungumza, pale ugeni kutoka Umoja wa Wanamichezo wa
Mpira wa Miguu kutoka FC GRACE UNITED STATES ulipomtembelea leo Ofisini
kwake Mjini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni
kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania ulioongozwa na Rais wa Chama
hicho Ndg. Mwadini Jecha (katikati) na Mratibu wa Mawasiliano Ndg. Anne
kilimo (kushoto) uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Spika
wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya
pamoja na Washindi wa Medali za Dhahabu katika Mashindano ya kimataifa
ya Mazingira na Sayansi yaliyofanyika hivi karibuni nchini Marekani.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shule ya Wavulana ya Feza Ndg. Ibrahim
Rashid, anaefuata ni Ndg. Rashid Kikwete, kulia ni Mhe. Hawa Ghasia, wa
pili kulia ni Ndg. Kassi Nkamia na watatu kulia ni Ndg. Abdallah Rubeya,
waliotembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (katikati waliokaa) akiwa katika
picha ya pamoja na ugeni kutoka Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania
ulioongozwa na Rais wa Chama hicho Ndg. Mwadini Jecha (kushoto waliokaa)
baada ya kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Naibu
Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Rais wa
Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Mwadini Jecha (katikati) pale
ugeni kutoka Chama hicho ulipomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma,
kushoto ni Mratibu wa Mawasiliano, Anne Kilimo.
COMMENTS