Na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Mhe Kisare Makori ameamuru kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 ...
Na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Mhe Kisare Makori ameamuru
kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 Mweka hazina wa Kikundi cha ulinzi
shirikishi Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo Ndg Raymond Mlimba kwa kushindwa
kuonyesha vielelezo vya matumizi ya fedha alizopewa kupeleka Benki.
Agizo
Hilo limetolewa wakati wa Mkutano wa Mkuu wa Wilaya na wananchi wa Mtaa
huo Mara baada ya kumtaka Mweka hazina huyo kutoa majibu kuhusu
matumizi ya fedha zilizotakiwa kuwekwa Bank kwa ajili ya malipo ya
vijana wanaounda umoja wa kikundi Cha ulinzi shirikishi.
Kutokea
kwa kadhia hiyo kulijili Mara baada ya Kila mwananchi aliyesimama
kuzungumza kulalamikia matukio ya uhalifu hususani wizi ambayo yameanza
kutokea mara kwa mara katika mtaa huo mara baada ya vijana waliokuwa
wakishiriki kwenye ulinzi shirikishi kutolipwa fedha zao kwa mujibu wa
makubaliano.
Mweka Hazina huyo alishindwa kuonyesha
vielelezo vya uwekaji na utoaji wa fedha Bank ambapo aliwaeleza wananchi
mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kuwa amehifadhi jumla ya shilingi
milioni 1.2 ilihali Fedha zilizotajwa na Ofisa Mtendaji wa Mtaa zilizopo
Bank ni Shilingi laki sita pekee.
Mhe Makori pia
amemuagiza Mwenyekiti wa Mtaa wa Msewe kuitisha mkutano wa Mtaa ili
kufanya makubaliano ya kuunda kamati ya Ulinzi shirikishi kwani hiyo ni
njia rahisi ya kukomesha matukio ya ukabaji na uporaji ambayo
yameshamiri kutokana na umbali wa vituo vya Polisi.
Mhe
Makori amepokea maombi mengine ya wananchi hususani Ujenzi wa Kituo Cha
Polisi, Kero ya maji machafu, Ombi la Zahanati ya Msewe kupandishwa
hadhi na kuwa Kituo Cha afya, Sambamba na Ombi la kuboreshwa madarasa ya
shule ya Msingi Msewe na mazingira yake ambapo ameahidi kuyatolea
majibu hivi karibuni.
Alisema kuwa serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Rais Mhe Dkt John Pombe Magufuli inadhughulika na
kuwatetea wanyonge kwa kusikiliza kero zao na kuzitatua sambamba na
kusukuma gurudumu la maendeleo kwa watanzania wote pasina kujali itikadi
ya vyama vyao ama dini zao.
Ziara ya Mkuu wa Wilaya Mhe
Kisare Makori ni muendelezo wa kuzuru katika Mitaa ya Wilaya ya Ubungo
ili kuwafikia wananchi mahali walipo na kuzitambua changamoto
zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.
IMETOLEWA NA;
OFISI YA MKUU WA WILAYA YA UBUNGOMkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Mwenyekiti wa Mtaa wa Msewe, Kata ya Ubungo Ndg Idan Fransis Msuya akizungumza wakati wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Msewe, Kata ya Ubungo wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati akihutubia Mkutano uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori (Katikati), Ofisa Tarafa ya Kibamba Ndg Beatrice Mbawala (Kushoto) na Mwenyekiti wa Mtaa wa Msewe (Kulia) Ndg Idan Fransis Msuya Wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi MseweOfisa Tarafa ya Kibamba Ndg Beatrice Mbawala akisisitiza Jambo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori kuhutubia Mkutano uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe.Bi Manase Msajigwa Konongwa Mkazi wa Mtaa wa Golani akieleza kadhia ya wizi iliyowahi kumkumba hivi karibuni mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Msewe, Kata ya UbungoBi Mariam Makubi Mkazi wa Mtaa wa Msewe akieleza kero yake mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Msewe Kata ya Ubungo.Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo wakimlaki Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es salaam Mhe Kisare Makori mara baada ya Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe kumalizika.Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Msewe Kata ya Ubungo wakimlaki Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Mhe Kisare Makori mara baada ya Mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya shule ya Msingi Msewe kumalizika.

COMMENTS