“Kupitia wataalam wa afya waliopo katika mipaka ya nchi serikali itakuwa ikitoa taarifa za mara kwa mara ya namna uzuiaji wa ugon...
“Kupitia
wataalam wa afya waliopo katika mipaka ya nchi serikali itakuwa ikitoa taarifa
za mara kwa mara ya namna uzuiaji wa ugonjwa huo kwa wananchi na wanapata elimu
ya kutosha ya kujikinga na virusi vya Ebola”, alisema Waziri Ummy.
Waziri Ummy aliongeza kuwa wananchi wanashauriwa kutoa
taarifa pamoja na kupata elimu kuhusu ugonjwa wa Ebola kwa kupiga simu namba
117 na kupata huduma bila ya malipo kwa mitandao yote.
Aliongeza kuwa Serikali imeendelea kutoa mafunzo kwa
wataalamu wake walioko mipakani ikiwa ni pamoja na utoaji wa vifaa vya
kujikinga na ugonjwa huo pamoja na vidonge kwa wataalamu hao walioko mipakani.
“Serikali tayari imeagiza mashine nne kwa ajili ya
kufanya vipimo katika mipaka yetu pamoja na viwanja vya ndege na bandari zetu
na tutahakikisha kila mgeni anayewasili nchini kutokea Congo anasajiliwa,”
alisema Waziri Ummy.
Ugonjwa wa Ebola unasababishwa na kugusa majimaji
yanayotoka kwa mgonjwa mwenye virusi vya Ebola na mizoga na dalili za ugonjwa
huu zinatokea baada ya siku mbili pindi mgonjwa anapopata maambukizi ya ugonjwa
huo zikiwemo kutokwa na damu sehemu za puani, masikioni na homa kali.
COMMENTS