Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba wa pili kushoto akitoa Maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Wizar...
Waziri
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba wa
pili kushoto akitoa Maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Wizara yake
wakati wa Kikao cha cha maandalizi ya mwisho cha kupitia Bajeti ya
Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla ya kuiwasilisha Bajeti ya
Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto (kwake) ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo
Mhandisi Hamadi Masauni na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest
Rwegasira (kulia), Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa
Wizara mjini Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu aliyenyanyua mkono akitoa ufafanuzi wa jambo fulani kuhusu bajeti ya Jeshi la Polisi nchini mbele ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siku ya Jumanne. Kikao
hicho kilichowashirikisha Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo na Maafisa
Mipango wa Wizara kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo mjini Dodoma.

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akipokea
taarifa mbalimbali zilizotolewa na watendaji wakuu wa Wizara yake
wakati wa Kikao cha Maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara yake, kabla
ya kusomwa kwa Bajeti ya Wizara yake katika Vikao vya Bunge la Bajeti
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumanne. Kushoto (kwake) ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Masauni, Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa wizara mjini Dodoma.

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini,
Dkt. Juma Malewa (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi mbele ya Waziri wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kuwasilishwa kwenye Vikao
vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siku ya
Jumanne.

Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Thobias Andengenye akitoa ufafanuzi kuhusu Jeshi lake mbele ya Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wakati wa Kikao cha
maandalizi ya mwisho ya kupitia ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika
Wizara hiyo, kabla ya Bajeti ya Wizara hiyo kusomwa kwenye Vikao vya
Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, siku ya Jumanne.
(PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI)
COMMENTS