Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika ...
Add caption |
Umoja wa Mataifa nchini umeendelea na
hekaheka za ufundishaji wa machampioni wa kusaidia kueneza malengo 17 ya
dunia yanayohusu maendeleo endelevu.
Miongoni mwa mambo yaliyofanywa siku ya pili ya ziara ya Mratibu Mkazi
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo
(UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwa mkoa wa Kilimanjaro na Arusha ni
kuendelea kwa mkutano wa vijana unaoakisi Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
mjini Arusha , na kuoongoza kampeni ya elimu ya maendeleo endelevu
katika Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU).
Akiwa MoCU Rodriguez aliwataka vijana kujikita katika kuyaelewa malengo
ya dunia na kuyafanyia kazi.
Ofisa
wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akiitambulisha meza kuu kwa
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) wakati wa kutoa uelewa
juu ya malengo ya dunia chuoni hapo.[/caption]
Akifafanua mchango wa vijana katika kufanikisha malengo hayo, Matibu
huyo alisema: “Mchango wa vijana ni muhimu katika kufanikisha malengo
endelevu kufika mwaka 2030; hivyo ni vyema kila kijana akafahamu na
kuwafundisha vijana wenzie malengo hayo muhimu.”
Septemba 2015, wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa walikubaliana juu ya
malengo mapya ya dunia, malengo ya maendeleo endelevu.
Malengo hayo yanatarajiwa kufanyiwa kazi katika kipindi cha miaka 15
ijayo na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii, uchumi na mazingira kwa
namna ya kuwa endelevu.
Wakati Umoja wa Mataifa (UN) mwaka jana ukiadhimisha miaka 71 tangu
kuanzishwa kwake, Mratibu huyo wa mashirika ya Umoja wa Mataifa aliahidi
kuwatumia vijana katika utekelezaji wa malengo yake 17 ya maendeleo
kutokana na idadi yao kubwa kubwa zaidi ya asilimia 67 na pia kwa kuwa
wao ndio wanaobeba hali ya baadaye ya nchi hii.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza juu ya malengo ya
maendeleo endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi
(MoCU) walioshiriki semina ya uelewa wa malengo hayo 17 ya dunia
iliyofanyika chuoni hapo.
Aidha alisema ili kufanikisha hilo, UN pamoja na mashirika mengine
itatoa mafunzo ya vitendo kwa vijana zaidi ya 50,000 ifikapo mwaka 2017
ambao wataingizwa katika mpango wa utekelezaji wa malengo hayo.
"UN itaendelea kushirikiana na vijana pia itatoa elimu ya vitendo.Hadi
sasa vijana zaidi ya elfu 20,000 wamepewa mafunzo na wanatambua malengo
hayo, na kwamba
UN na wadau wengine wanatarajia kufundisha vijana zaidi ya 50, 000
ifikapo mwaka 2017, ili ifikapo 2030 vijana wengi wawe wanajua malengo
hayo na namna ya kuyatekeleza," alisema.
Ofisa
wa dawati la Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere akitoa neno kwa wanafunzi wa
MoCU wakati wa semina ya uelewa wa Malengo ya Dunia iliyofanyika chuoni
hapo.
Amesema miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa kwa vijana hao ni pamoja na
jinsi ya kufanikisha malengo 17 ya maendeleo endelevu na jinsi ya vijana
watakavyoweza kujiajiri.
Akiwa Moshi jana, alizungumza na wanachuo na wahadhiri ambapo katika
chuo hicho cha MoCU 460 walipatiwa mafunzo na pia walimhoji mambo
mbalimbali yanayohusu Umoja wa Mataifa na malengo ya dunia ya maendeleo
endelevu.
Kwa mafunzo yaliyofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha
Umoja wa Mataifa ulifua vijana 50 ambao ni machampioni.
Mkuu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu akisisitiza jambo
kwa wanafunzi wa MoCU wakati wa semina ya uelewa wa malengo ya dunia
iliyofanyika chuoni hapo.
Aidha idadi ya vijana waliofikiwa na mafunzo hayo kwa kuambukizana
wameongezeka na kufikia zaidi ya elfu 20.
Tangu kuzinduliwa kwa kampeni hiyo na mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini Alvaro Rodriguez, mwaka jana vijana zaidi wamepata elimu
katika maeneo yao kwa kupitia machampioni wa malengo.
Kwa sasa Tanzania imehusisha malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs)
kwenye mpango wa maendeleo wa miaka mitano.
Picha
juu na chini ni wanafunzi na walimu MoCU walioshiriki semina ya uelewa
wa malengo ya dunia iliyoendeshwa na Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini chuoni hapo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na Eng.
Salvatory Matemu kutoka Ofisi ya RC Kilimanjaro huku Ofisa wa dawati la
Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Idara ya Ushirikiano wa
Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Ngusekela Karen Nyerere (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi
wa Rasilimali watu MoCU, Daud Massambu wakielekea kwenye zoezi la picha
ya pamoja.
Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU.
Picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa MoCU.
Mkuu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kushoto)
katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa UN Chapter MoCU, Isaac Evarist
(kushoto) pamoja na wanafunzi chuoni hicho.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwapiga msasa machapioni wa
malengo ya dunia katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha.
Mmoja
wa machampioni akipitia kipeperushi kinachoelezea kwa kina malengo 17
ya dunia wakati wa mafunzo yaliyoendeshwa na Mratibu Mashirika ya Umoja
wa Mataifa nchini (hayupo pichani).
Mratibu
wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia)
akisikiliza swali kwa umakini kutoka kwa Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu
cha Tumaini Makumira mkoani Arusha, John Semindu wakati wa mafunzo kwa
machampioni wa SDGs chuoni hapo.
Mmoja wa machampioni wa Makumira akiuliza swali kwa Mratibu wa Mashirika ya UN nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).
Picha
juu na chini ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
akikabidhi vyeti kwa machampioni wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)
wa Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha na Taasisi ya Uhasibu
ya Arusha (Institute of Accountancy Arusha -IAA) walioshiriki mafunzo
hayo.
Ofisa
wa Mawasiliano na Ushirikiano NUNV kutoka Ofisi ya Mratibu Mkazi wa
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Didi Nafisa akimuelekeza jambo mmoja wa
machampioni wa malengo ya dunia wakati wa mafunzo yaliyofanyika Chuo
Kikuu cha Tumaini Makumira mkoani Arusha.
COMMENTS