Makamu Rais wa Kampuni ya Star Media (Tanzania) Limited Zuhra Haif Fazal na Mkurugenzi wa Tekinolojia na Uendeshaji wa Benki TPB Jem...
Baadhi ya wafanyakazi wa Startimes media Tanzania (Ltd) na wageni wakiwa katika hafla hiyo wakati mmoja akiuliza swali. |
Wafanyakazi wa TPB Bank, Startimes media Tanzania (Ltd) na wageni wakiwa katika hafla hiyo. |
STARTIMES TANZANIA PARTNERS WITH TPB BANK
Dar es Salaam,
Star Times Tanzania, - the largest pay TV Company, has today announced a partnership with TPB Bank Plc (TPB) to allow customers to purchase high quality digital TV sets with decoder inside through TPB Bank loan. The loan will be in the form of Buy today, pay the money within 12 months.
The partnership will make it possible for Star Times customers to pay for their Digital TV not only through one time payment but also through 12 months installment at TPB Bank and customers in five region which are Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Arusha and Mbeya can access this service where there is TPB Bank branches across those region.
Speaking at the launch, the Star Times Corporate Manager, Mr. Antony Katunzi said “this partnership clearly demonstrates the revolutionary role that a Bank and a Pay TV company can play while simplifying payments for their customers and communities in general which will enable every family to own Star Times digital TV”
On his part, TPB Marketing Manager Mr. Amos Kasanga explained that the bank was proud to work with Star Times by providing affordable loans which will be available in five regions to start with, hoping that with time the loans will be available in other regions. This method is convenient and easy for customers to use.
“I am particularly happy today as we launch yet another product that brings together two giant companies in Tanzania, which will provide a platform that will enable our customers and every Tanzanian family to own Digital TV and to enjoy digital life through getting different content from every corner of the world” said Kasanga.
With this move, both Star Times and non Star Times customers can pay by installment Star Times digital TV through TPB branches. Tanzanians in both urban and rural areas can now easily manage to own digital TV depending on customer need and financial capability.
Different models of digital TVs will be available for customers who will be interested in the loan depending on their life standard and their needs. There are 24 inch, 32 inch and 40 inch TV sets with the price ranging from Tsh 45,000, to Tsh99, 000 payment for twelve month (12).
About StarTimes
StarTimes is the leading digital-TV operator in Africa, serving nearly 10 million subscribers and covering 90% of the continent's population with a massive distribution network. StarTimes owns a featured content platform, with 440 authorized channels consisting of news, movies, series, sports, entertainment, children's programs, fashion, religion etc. The company's vision is "To enable every African family to afford and enjoy digital TV" StarTimes achieves this by combining satellite and terrestrial DTV systems to provide an open and secure digital wireless platform. The company provides a robust signal transmission service for public and private broadcasters, offers consumers outstanding Pay-TV programs, mobile multimedia, wireless Internet connectivity and convenient online services including checking TV guide; watching free live football ; chatting with celebrities and friends.
For Media Queries
Mr., Juma Mchina Sharobaro Suluhu
Public Relations and Marketing Manager, Startimes Tanzania
TEL: 255758828277
EMAIL:tangjy@startimes.com.cn
STARTIMES YAINGIA UBIA NA TPB BANK Plc (TPB)
Kampuni ya startimes imeingia ubia na benki ya TPB kwa lengo la kuwakopesha wateja televisheni za kidigitali kwa awamu kupitia mkopo ambao utamwezesha mteja kulipa mpaka miezi kumi na miwili kutoka benki ya TPB.
Ubia huu unamwezesha mteja wa startimes kulipia kwa njia rahisi zaidi televisheni ya kidigitali sio tu kwa mara moja bali kwa awamu kupitia Benki ya TPB, na wateja wataweza kuipata huduma hii katika mikoa mitano ambayo ni Dar es salaam, Dodoma, Mwanza Arusha na Mbeya ambapo kuna matawi ya Benki hiyo.
Akiongea katika uzinduzi, Meneja Mahusiano wa StarTimes, Bw.Antony Katunzi alisema, “Ushirikiano huu unaashiria wazi mapinduzi ambayo Benki na Kampuni ya Televisheni zinaweza kuleta, kwa kurahisisha ulipiaji kwa wateja wao na jamii kwa ujumla ili kuwezesha kila familia kumiliki luninga ya kidigitali ya StarTimes”.
Naye Amos Kasanga, Meneja Masoko wa Benki ya TPB amesema benki hiyo imekubaliana na StarTimes kutoa mikopo hiyo midogo kwenye mikoa mitano ambapo huduma hiyo itapatikana. Njia hii ni rahisi zaidi kwa wateja kutumia.
“Najisikia furaha kubwa leo tunapozindua njia nyingine ambayo inazileta pamoja kampuni hizi kubwa mbili Tanzania, na hii itatoa fursa kwa wateja na kila familia ya kitanzania kumiliki luninga ya kidigitali na kufurahia maisha ya kidigitali kwa kupata vipindi mbali mbali kutoka kila kona ya dunia”
Kwa hatua hii, wateja na wasio wateja wa StarTimes, wote wanaweza kulipia luninga za kidigitali za StarTimes kwa awamu kupitia matawi ya Benki ya TPB. Watanzania waishio mijini na vijijini sasa wataweza kumiliki luninga za kidigitali kwa urahisi, kulingana na mahitaji na uwezo wao kifedha.
Tunayo matoleo mbalimbali ya luninga za kidigitali kwa ajili ya wateja wetu kulingana na mahitaji na uwezo wao. Tuna luninga ya inchi 24 kwa Tsh. 45,000/=,kwa kila mwezi kwa miezi kumi na miwili (12),inchi 32 Tsh 64,000/= na inchi 40 kwa Tsh. 99,000/= .
Kuhusu StarTimes
StarTimes ni kampuni ya Televisheni za kidigitali inayoongoza Afrika, huku ikihudumia karibia wateja milioni 10 na kufikia 90% ya bara hilo kwa mtandao ulioenea zaidi. Pia StarTimes ina uwanda maalumu wa vipindi, ikiwa na chaneli 440 zikiwamo chaneli za habari, filamu, tamthiliya, makala, sayansi, vipindi vya watoto, mitindo, dini na kadhalika. Dhumuni ya kampuni ya StarTimes ni “kuwezesha kila familia ya kiafrika kumiliki na kufurahia televisheni za kidigitali”. StarTimes inafanikisha hilo kwa kuunganisha mifumo ya satelaiti na televisheni za antenna kutoa huduma salama isiyotumia nyaya. Kampuni ya StarTimes pia inatoa huduma ya kusafirisha masafa (signal transmission) kwa kampuni za matangazo za umma na binafsi, huduma madhubuti ya vipindi vya televisheni za kulipia (Pay-TV), Vifaa-simu, mawasiliano ya intaneti, na huduma safi za televisheni kama vile kutizama mlolongo wa vipindi; kutizama mpira bure; kuchati na marafiki pamoja na watu maarufu.
Kwa Maswali
Mr. Juma Mchina Sharobaro Suluhu
Meneja Mahusiano na Masoko, StarTimes Tanzania.
TEL: 255758828277
EMAIL:tangjy@startimes.com.cn
COMMENTS