Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itaendel...
Na
Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa itaendelea
kuhamasisha Halmshauri zote nchini
kununua viuadudu vya kibailojia kwa ajili ya kuua viluilui vya mbu waenezao
Malaria vinavyotengenezwa na kiwanda cha Biotec product cha Kibaha.
Hayo
yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangala wakati akijibu swali la Mbunge wa Gando
Mhe.Othman Omar Haji.
“Viuadudu
hivi bimeanza kutengenezwa kuanzia mwezi Desemba 2016 na kwa sasa uhamasishaji
huu unaendelea na endapo viuadudu ivi
vitatumiwa vizuri vitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kiwango cha maambukizi
ya Malaria nchini”,Alisema Mhe.Kigwangalla.
Aidha
amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Ushirikiano na Serikali
ya Cuba imeendelea kushirikiana katika mambo mengi ikiwemo pamoja na Sekta ya
Afya tangu mwaka 1986 mkataba uliposainiwa kati ya Serikali hizi mbili.
Kupitia
mkataba huo Serikali ya Tanzania imekuwa ikipokea madaktari bingwa kutoka Cuba
ambao wamekuwa wakifanya kazi katika Hospitali za Muhimbili,Hospitali ya Rufaa
ya Kanda Mbeya , Hospitali Tumbi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma.
Mbali
na hayo amesema kuwa Madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma mbalimbali za
kibingwa kwa wananchi na kuwajengea uwezo madaktari wanaofanya nao kazi katika
Hospitali hizo.
Aidha
kwa kushirikiana na kampuni ya Labiofarm ya Cuba,Serikali imeweza kujenga
kiwanda cha kutengeneza viuadudu ivyo na Serikali ya Cuba imeleta wataalamu.
Kiwanda
icho cha Biotec cha kibaha kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 2.5 za
viuatilifu vya kuua viluilui vya mbu
waenezao Malaria kwa mwaka.
COMMENTS