NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI
HomeJamii

NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kuto...

SPIKA NDUGAI, KATIBU WA BUNGE, NDG. KAGAIGAI WATEMBELEA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII
MPANGO WA UENDESHAJI WA KIJINSIA KWA AJILI YA MWITIKIO WA UKIMWI TANZANIA BARA WATAMBULISHWA RASMI KWA MKOA WA SINGIDA
HITILAFU YA MFUMO WA KUPOKELEA GESI KINYEREZI I, TATHIMINI YAONYESHA MATENGENEZO MAKUBWA YANAHITAJIKA.

NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani Tanga (NHIF) unakusudia kuwafikia wananchi kwenye vijiji na kata mbalimbali mkoani hapa ili kutoa elimu juu ya umuhimu wa huduma ya afya kwa watoto (Toto Afya  Kadi) ambapo uelewa wake umekuwa sio mzuri.


Hayo yalisemwa na Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
(NHIF) Ally Mwakababu (Pichani Juu)wakati akizungumza na mtandao huu
ofisini kwake ambapo alisema wameamua kufanya hivyo ili kuipa uelewa
jamii kuhusiana na umuhimu na faida za huduma hiyo.


Alisema wakiwa huko watapita kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo mashuleni
na kufanya mikutano ya nje kwa wananchi ili kuweza kuwapa uelewa juu
manufaa ya kuwaingiza watoto hao kwenye mfuko huo.



“Unajua hii huduma Toto Afya Kadi hasa kwa maeneo ya vijijini uelewa
wake umekuwa sio mzuri hivyo sisi tumepanga kuanza kuhamasisha na kuipa
uelewa jamii ili waweze kuitambua na kujiunga nayo “Alisema.



“Nia kubwa ni kutaka kuona jamii waliochini ya miaka 18 wana jiunga na
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwani itawasaidia kupunguza gharama za
matibabu kwa sababu akishajiunga anaweza kupata matibabu bure “Alisema.


Sambamba na hilo alisema pia hivi sasa wanaihamasisha jamii kuendelea
kujiunga nao ikiwemo wajasiriamali na vikundi vilivyosajiliwa ili kuweza
kunufaika na huduma zinazotolewa na mfuko huo.


“Lakini pia tunaendelea kuhamasisha wakina mama kujiunga na mradi wa KFW
mradi ambao unaendelea kwenye mikoa ya Mbeya na Tanga  kwani
itawasaidia kupata matibabu pindi wanapokuwa wameugua “Alisema.


Akizungumzia changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo, Meneja huyo
alisema ni uelewa mdogo wa wananchi hasa maeneo ya vijijini na
katakuchangamkia fursa za mfuko huo.


(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI
NHIF TANGA KUPELEKA HUDUMA YA TOTO AFYA KADI VIJIJINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiN47CpO4Sz0cpchzyXV3gsO46Ul5bsvysV4QdmarGCYHvu54P4EK1laFDiJDgZ4_RkFQtA3CQA7YGWQte91XitgxG3FVEdb4qBKklhVx-h4GRvGtCjNv8KJb3VZTePZRAKI4R1zdLjOU8W/s640/2.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiN47CpO4Sz0cpchzyXV3gsO46Ul5bsvysV4QdmarGCYHvu54P4EK1laFDiJDgZ4_RkFQtA3CQA7YGWQte91XitgxG3FVEdb4qBKklhVx-h4GRvGtCjNv8KJb3VZTePZRAKI4R1zdLjOU8W/s72-c/2.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/nhif-tanga-kupeleka-huduma-ya-toto-afya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/nhif-tanga-kupeleka-huduma-ya-toto-afya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy