Mnufaika wa Airtel FURSA bidhaa zake ziko sokoni mikoa zaidi ya mitano Mradi wa Airtel Fursa umeendelea kufanikiwa kwa kuendele...
Mnufaika wa Airtel FURSA bidhaa zake ziko sokoni mikoa zaidi ya mitano
Mradi
wa Airtel Fursa umeendelea kufanikiwa kwa kuendelea kuwezesha vijana
nchini ambapo mmoja kati ya waliowezeshwa mwaka jana Bi Threria
Maliatabu mkazi wa Mbagala jijini Dar es Saalam ameelezea jinsi mradi
huo ulivyomuwezesha kukuza kipato na kupata mafanikio ya kuanza kujenga
nyumba yake binafsi, kujinunulia shamba la eka 2 huku akiwaasa vijana
wenzake nchni na wale wote waliowezeshwa na Airtel FURSA kuchangamkia
fursa hizi pindi zinapotokea.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es saalam , Bi Maliatabu ambaye
anajishughulisha na biashara ya uchoraji wa picha za sanaa alisema “
najivunia sana kuwa mmoja kati ya vijana walioshikwa mkono na Airtel
Fursa kwa sababu program hii imeweza kunitoa kutoka niliopokuwa hadi
kufika kwenye haya mafanikio niliyo nayo leo.
Kwakweli
nimekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuboresha kiwango cha bidhaa
zangu , nimefanikiwa kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba vinne na
pia nimeweza kukunua shamba la eka 2 Mkuranga mkoa wa pwani. lengo langu
ni kuanzisha shughuli za kilimo ili kutanua wigo wa biashara yangu
lakini pia kuendelea na shughuli yangu ya uchoraji nayoifanya kwa sasa”
Aidha
Maliatabu alifafanua kuhusu changamoto mbalimbali katika biashara
ikiwemo masoko ya nje , usafiri wa kusambaza bidhaa zake huku akieleza
kuwa baadhi ya changamoto hizi ameshaanza kuzishughulikia na kuomba
wadau mbalimbali kuweza kumsaidia.
“Nimeweza
kuongeza masoko yangu na kufikia masoko ya Zanzibar, Moshi , Arusha na
Dar, na kwa sasa niko katika mchakato wa kupeleka bidhaa zangu nchini
Sweeden na Italy. Mipango hii ikikamilika kwakweli nitakuwa nimefurahi
kufikia malengo yangu na naamini nitafanya vizuri zaidi na kukuza kipato
changu zaidi. Natoa wito kwa vijana wenzangu kujituma na kufanya kazi
kwa bidiii na kutafuta fursa mbalimbali na kujikita kwenye ujasiriamali
badala ya kusubiri ajira ambazo zimekuwa ni changamoto”.
Akiongea
kuhusu mafanikio haya, Meneja Huduma kwa Jamii, Bi Hawa Bayumi alisema ,
tunafarijika na kujisikia fahari kuona jinsi gani program hii imeweza
kuwainua vijana hawa wajasiriamali wenye nia ya kukuza kipato na kufikia
malengo yao. Theresia Maliatabu ni mfano wa kuigwa, alipowezeshwa
alijiongeza na kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa. Nawaasa vijana
wajitume na kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza wazitumie vizuri
ili kuleta tija kwenye maisha yao, familia zao na taifa kwa ujumla.”
Theresia
Maliatabu ni moja kati ya vijana waliochagulia kuwa kati ya
wafanyabiashara wadogo wadogo watakaonufaika na mpango wa Airtel FURSA
na kupatiwa vitendea kazi zikiwemo , ubao wa kuchorea, vifaa vya
kuchorea na computer, mafunzo ya ujasiriamali na kutengenezewa kipindi
maalumu cha Television kilichoonyesha safari yake katika biashara
ambavyo vimemsaidia kukuza biashara yake. Airtel kupitia mpango wake wa
Airtel fursa imewezesha vijana takibribani 5000 kwa kuwapatia mafunzo ya
ujasirimali na baadhi yao kupata vitendea kazi ili kuboresha biashara
zao.
Theresia
Maliatabu, mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa akimsikiliza mteja wakati
alipohudhuria maonyesho ya bidhaa na kuonyesha kazi ya uchoraji wa picha
za Sanaa anazozifanya hivi karibuni.
COMMENTS