NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari MGOMBE urais wa Ufaranasa, mwanamama Marine Le Pen,(48), amerushiwa mayai na waandam...
NA K-VIS BLOG/Mashirika ya Habari
MGOMBE
urais wa Ufaranasa, mwanamama Marine Le Pen,(48), amerushiwa mayai na
waandamanaji dakika chache kabla ya kuongea na waandishi wa habari.
Walinzi
wake walilazimika kumuondoa kwa haraka huku wakimfunika baada ya mayai
kuvurumishwa na waandamanaji hao wanaopinga sera za mgombea huyo ambaye hataki
wahamiaji.
Tukio hilo
lililotokea Mei 4, 2017, limekuja siku moja baada ya kushiriki katikammdahalo
wa TV na mpinzani wake, Emmanuel Marcon.
Hata hivyo
hakuna yai lililompata, baada ya walinzi wake kujenga “ukuta” na kumuondosha
kwa haraka kwenye eneo la tukio.
Kiasi cha
waandamanaji wapatao 50, walikuwa wamejipanga, wakati Mama Le Pen alipowasili
kwenye kampuni ya usafirishaji kwenye mji wa Magharibi wa Dol-de-Bretagne na
kuanza kubuirumisha mayao huku wakipiga kelele za fashist.
Bibi Le Pen akiwasili eneo alikorushiwa mayai.
Waandamanaji wanaopinga sera za Bbi Le Pen
Walinzi wa Bibi Lepen, "wakijenga ukuta" kumuokoa na "makombora" ya mayai
Bi Le Pen akisindikizwa na walinzi wake
Emmanuel Marcon
COMMENTS