Mkuu wa Kitengo cha Fedha-Tigo Pesa katika kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Christopher Kimaro akiongea na waandishi wa habari wakat...
Dar es Salaam, Mei 10, 2017- Watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa wamelipwa jumla ya 5.48bn/- kama faida ya gawio inayolipwa kila mwaka na kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tanzania.
Hii ni mara ya 12 Tigo inagawa malipo ya robo mwaka kwa watumiaji wa huduma ya fedha kwa simu tukio ambalo imekuwa ni kampuni ya kwanza ya simu kufanya hivyo duniani tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo Julai 2014.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo inaonesha kuwa kampuni hiyo inalipa malipo hayo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka kilichoishia Machi 31, 2017
Kwa mujibu wa Mkuu Kitengo cha Fedha, Tigo Pesa Christopher Kimaro kwa ujumla watumiaji wa Tigo Pesa wameshapata 63.58bn/- kama faida ya gawio lao tangu kuanza kwa mpango huo ,mwaka 2014. Malipo hayo ni faida inayotoka katika akaunti za Mfuko wa Tigo Pesa ambazo zimo katika mabenki makubwa ya biashara nchini.
Wanaopokea gawio hilo ni pamoja na wateja binafsi, mawakala wa rejareja, mawakala wakubwa na washirika wengine wa kibiashara wa Tigo Pesa ambao kila mmoja anapokea malipo hayo kulingana na kiasi cha thamani ya fedha-elektroniki waliyonayo kila siku ndani ya pochi zao za Tigo Pesa,” alisema Kimaro katika taarifa hiyo.
“Tunayo furaha kutangaza gawio hili la faida kwa mara ya 12 mfululizo. Hili liko katika mikakati yetu ya kujikita kutoa na kufikiwa kwa huduma za kifedha kwa wateja wetu na nchi kwa jumla kupitia huduma zetu za Tigo Pesa,” alisema Kimaro.
Alibainisha kuwa kuongezeka kwa faida katika Tigo kunaboresha mazingira ya soko na kukua kuliko imara kwa idadi ya watumiaji wa Tigo Pesa. Tigo Pesa hivi sasa ina mtandao mkubwa wa wafanya biashara zaidi ya 80,000 kote nnchini.
“Tigo ni kampuni ambayo bado inakua kwa kasi ikiwa ni kama motisha kwa uaminifu wa chapa Tigo iliyoamua mwaka 2014 kuwazawadia wateja wake kupitia faida ya gawio, na wakati huo huo ikiwekeza kwa kadri inavyoweza katika kukua zaidi,”alisema Kimaro.
Kama ilivyokuwa awali gawio hilo kwa wateja kwa mujibu wa Kimaro linakokotolewa kulingana na wastani wa kila siku wa fedha za mteja zilizomo katika pochi yake ya simu ya Tigo Pesa na kwamba kugawanywa kwa gawio hilo la faida upo katika Waraka wa Benki Kuu uliotolewa Februari 2014.
COMMENTS