Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa BAlozi Seif Ali Iddi akizungumza na wana CCM mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Maskani...
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa BAlozi Seif Ali Iddi akizungumza na wana CCM mara
baada ya kuweka jiwe la msingi la Maskani ya CCM ya Tuheshimiane yenye
wanachama 105 walioamua kuiacha CUF na kujiunga na CCM hapo katika
Kijiji cha Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Masheha na
Wakuu wa Wilaya hawana haja ya kutishika wakati wanapotekeleza majukumu
yao waliyokabidhiwa na Serikali hasa suala zima la uandikishaji wa
vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi.
Alisema
viongozi hao wanapaswa kuhakikisha kwamba mtu asiye na sifa ya
kujiandikisha kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho hivyo hastahiki kupewa
ili kuiepusha Serikali kupata hasara ya kutengeneza vitambulisho ambavyo
baadaye vinaharibika bila ya kuchukuliwa na wale waliojiandikisha.
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya
Taifa ya Chama cha Mapinduzi alitoa kauli hiyo mara baada ya kuweka jiwe
la msingi la Maskani ya CCM ya Tuheshimiane yenye wanachama 105
walioamua kuiacha CUF na kujiunga na CCM hapo katika Kijiji cha
Makangale Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Balozi
Seif alisema wapo vijana wengi waliojiandikisha kwenye vitambulisho vya
Mzanzibari Mkaazi hasa katika Kisiwa cha Pemba wakitokea maeneo ya
Tanga Tanzania Bara na Mombasa Nchini Kenya wakielewa kwamba kitendo
chao ni kosa la jinai na ndio sababu zilizopelekea kushindwa kuchukuwa
vitambulisho hivyo baada ya kutengenezwa na hatimae kuitia hasara
Serikali.
Alionya
kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi pamoja na taasisi
zinazohusika itahakikisha kuwa mtu asiye na sifa kamwe hatapate fursa
hiyo na wale watakaoamua kufanya ujanja haitasita kuchukuwa hatua za
kisheria dhidi ya wahusika hao.
Balozi
Seif aliwapongeza Vijana hao wa Makangale kwa uamuzi wao wa kuacha
kuunga mkono vyama vya upinzani na kujiunga na Chama cha mapinduzi
chenye sera zinazotekelezeka sambamba na kuthamini watu wote bila ya
ubaguzi.
Alisema
Chama cha Mapinduzi kupitia Makamu Mwenyekiti wake upande wa Zanzibar
Dr. Ali Mohamed Shein kimeamua kutilia mkazo ufufuaji wa maskani nchini
ili kuongeza nguvu za chama kuanzia ngazi ya chini.
Alisema
Maskani zinarejeshwa tena baada ya kufifia katika kipindi cha kati
kutokana na chama cha Mapinduzi kuingiliwa na vijidudu Mtu vilivyoharibu
mpango huo wa uimarishaji wa Maskani za CCM Zanmzibar.
Mjumbe
huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu nya Taifa ya CCM aliwahakikishia
wanachama na wananchi hao wa Makangale kwamba Chama cha Mapinduzi kwenye
uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka kesho itavuna viti vingi Kisiwani Pemba.
“
Wembe iliyoutumia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mdogo wa mwaka
2002 Kisiwani Pemba na kufan ikiwa kupata viti sita unanolewa tena kwa
ajili ya kazi hiyo “. Alisema Balozi Seif.
Alisema
wana CCM wanapaswa kupania vilivyo kuumaliza upinzani hapa nchini na
dalili ziko wazi kwa vile wale waliokuwa wakiubeba upinzani katika
chaguzi zilizopita hivi sasa hawana tena nguvu za kufanya hivyo.
Katika
Kuunga mkono wanachama hao wa Maskani ya CCM ya Tuheshimiane Makangale
Balozi Seif aliahidi kumaliza kazi iliyobakia ya ujenzi wa Maskani ya
Wanachama hao baada ya kupiga mchango wa papo kwa papo na kupatikana
zaidi ya shilingi Milioni Tatu zilizoahidiwa pamoja na fedha taslimu.
Mapema
katika risala yao wana CCM Hao wa Tuheshimiane Makangale walisema
uamuzi wao wa kuiacha CUF na baadaye ADC na kujiunga na Chama cha
Mapinduzi haukuwa na ushawishi wowote.
Walisema
maamuzi yao yalizingatia zaidi kuridhika na vitendo na utekelezaji wa
ilani ya CCM chama ambacho kinajali watu wa rika, dini na makabila
yoyote yaliyopo hapa nchini.
Vinana
hao wa CCM waliwathibitishia Viongozi wa CCM wa ngazi zote kwamba
pamoja na changamoto zinazowakabili katika harakati zao za maendeleo
pamoja na kuimarisha Chama lakini kamwe hawatoyumba na wataendelea
kuiunga CCM kwa nguvu na muda wao wote.
Baadhi
ya Viongozi wa CCM alioahidi kuichangia ujenzi wa maskani hiyo ya
Tuheshimiane Makangale ni pamoja na Mh. Mohamed Aboud Mohamed, Mh. Dr.
Maua Daftari, Mh. Maida, Mh. Bihindi Hamad, Uongozi wa Wilaya ya
Micheweni pamoja na wanachama wengine wa kawaida kutoka sehemu mbali
mbali hapa Nchini.
COMMENTS