Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii. Bodi ya Wadhamini ya CUF kupitia wakili wao, Hashimu Mziray leo imewasilisha kusudio la kuk...
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Bodi
ya Wadhamini ya CUF kupitia wakili wao, Hashimu Mziray leo imewasilisha
kusudio la kukata rufaa kupinga uamuazi uliotolewa na mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu uliotupilia mbali kesi yao sababu CUF haina Bodi ya
wadhamini.
Bodi
hiyo inapinga uamuzi wa uliotolewa mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri ambapo maombi yao dhidi ya Mbunge wa Kaliua, Magdalena
Sakaya (CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma(CUF) na wenzao
sita yakuomba mahakama iwazuie kwa muda kujihusisha katika masuala ya
uongozi na kufanya mikutano ya chama.
Wakili
wa bodi ya Wadhamini ya CUF, Hashimu Mziray amesema wamewasilisha
kusudio hilo la kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na hakimu
Mashauri kwa kuwa si kweli kuwa CUF haina bodi ya wadhamini.Amedai kuwa
CUF IPO hai, inawabunge, madiwani, majengo, wanachama na kwamba msajili
wa vyama vya siasa hajakifuta.
ameongeza
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri hakulielewa tangazo la Wakala wa
Vizazi na Vifo (Rita) na kuiomba Mahakama Kuu itengue maamuzi ya Hakimu
Mashauri kwa kuwa ni batili.Mei 21 mwaka huu, Hakimu Mashauri alitoa uamuzi wa kuitupilia mbali kesi hiyo baada ya kusikiliza pande zote mbili.
Akitoa
uamuzi huo, Hakimu Mashauri alisema Joram Bashange ambaye aliapa katika
kiapo kuwa ni Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF aliapa uongo kwa
sababu bodi hiyo ilisha isha muda wake na kwamba pande zote mbili wana
maombi RITA ya kuomba usajili.ameongeza kuwa Bashange ni Katibu wa Bodi
ya Wadhamini ya CUF na kwamba yeye binafsi ndiye atabeba gharama za
kesi.
Katika
kesi hiyo Sakaya na wenzake walikuwa wakiwakilishwa na Wakili, Mashaka
Ngole huku bodi ya Wadhamini ya CUF ikiwakilishwa na Wakili Hashimu
Mziray.
Katika
pingamizi wajibu maombi wanadai maombi hayawezi kusikilizwa katika
mahakama hiyo kwa sababu yanashughulikiwa katika maombi namba 23/2016
yaliyopo Mahakama Kuu.Wanadai mwombaji hana miguu ya kusimamia kufungua
kesi dhidi ya wajibu maombi, maombi hayo hayana msingi kwa kushindwa
kubainisha jina la mwandishi wa masuala ya fedha hivyo wanaiomba
mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo kwa gharama.
Maombi
hayo yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura ni dhidi ya wajibu
maombi Sakaya, Nachuma, Thomas Malima, Omar Masoud, Abdul Kambaya,
Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jaffari Mneke.
Bodi
ya wadhamini ilikuwa inaomba mahakama itoe zuio la muda kuwazuia wajibu
maombi, mawakala wao au watu wao wowote kujihusisha katika masuala
yoyote ya uongozi au kufanya mikutano ya chama hicho, hadi maombi yao
hayo yatakaposikilizwa kwa pande zote husika.Wakili
Mziray aliomba maombi hayo yasikilizwe kwa haraka kwa madai kwamba
wajibu maombi wanataka kujiingiza katika kufanya mikutano ya chama
hicho, wakati hawana uwezo wa kufanya hivyo.
Bodi
hiyo ya wadhamini ya CUF iliamua kufungua kesi hiyo mahakamani hapo siku
moja baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba,
kutangaza kutengua nafasi tano za wakurugenzi wa chama hicho na
kutangaza majina mapya.
COMMENTS