MKURUGENZI WA JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATENDAJI WAKE
HomeJamii

MKURUGENZI WA JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATENDAJI WAKE

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Juma Kihamia alizungunmza na watumishi wa serikali katika kikao kilichofanyika mjini Arusha    ...

AGGREY&CLIFFORD YATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU, DAR
SERIKALI YAWEKA MIKAKATI YA KUWAONDOA VIJANA KATIKA MAZINGIRA HATARISHI ILI WASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII
RAIS DKT MAGUFULI AFUNGUA NYUMBA ZA MAKAZI ZA NHC IYUMBU DODOMA LEO



Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Juma Kihamia alizungunmza na
watumishi wa serikali katika kikao kilichofanyika mjini Arusha 
 

Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Juma Kihamia amefanya kikao na watumishi wa serikali katika Kata ya Muriety na Terati na kuzungumza mambo mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha utendaji kazi wao.

Kihamia amesema kuwa lengo hasa la kuonana na watumishi hao ni muendelezo wa ziara yake ya kutembela kila Kata na kuwakumbusha watumishi hao jinsi ya kuendana na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya Rais John Magufuli.

“”Siyo kwamba watumishi wangu wa Halmashauri hawafanyi kazi bali ni kuwakumbusha majukumu yao katika kutumikia wananchi hasa katika kasi ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu ambayo inatutaka tuwe karibu zaidi na wananchi wetu na Mimi kama Mtendaji mkuu lazima nisimamie kikamilifu “” Alisema Kihamia.

Vile vile amesema kuwa watendaji wa serikali wanatakiwa wajitume kwa nguvu zote wasisubiri mpaka viongozi wa juu wafike kwenye maeneo yao na wananchi walalmike wakati kuna kiongozi katika eneo hilo ambaye analipwa na serikali ili kusaidia wananchi.

“” Hatutaki Mwananchi atoke kwenye Kata mpaka kwa mkuu wa Mkoa au mkuu wa Wilaya wakati kwenda kumlalamikia masuala madogo madogo wakati kuna kiongozi ambaye tumemuweka ili atatue kero akitokea Mtumishi wa hivyo ajue kwamba hatoshi kuongoza wananchi “”Alisema Kihamia

Ameongeza kuwa kwa sasa anahakikisha huduma zinaboreshwa katika jiji la Arusha kwa kumjengea mtumishi uzoefu wa kufanya kazi bila kuogopa changamoto zilizopo na kuwa jasiri wakati anaongoza wananchi kwenye maeneo yao.

Hata hivyo amewagiza watumishi hao wa serikali wakiwemo watendaji kutekeleza kwa muda uliowekwa mambo muhimu kama vikundi vya vijana na Wanawake, kuainisha maeneo ya biashara na idadi yake ikiwemo mabango Na maduka yote, majengo na miradi viporo pamoja na kuainisha Yale maeneo yote ya wazi.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKURUGENZI WA JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATENDAJI WAKE
MKURUGENZI WA JIJI ARUSHA ATOA SEMINA KWA WATENDAJI WAKE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhy7bSSYtC_6gIidEeHQi6DKabmyotJaX9nRECUEPTL8mmm6P93jrTx9mi3ofYUSvR3L3Bi1nZ8arUBGkmhqYJzjvI_AVfhnxABX9T5sBX_OLPWkmSPvJAtxNTtDDS4nE6K1Ya4wRgzA-oG/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhy7bSSYtC_6gIidEeHQi6DKabmyotJaX9nRECUEPTL8mmm6P93jrTx9mi3ofYUSvR3L3Bi1nZ8arUBGkmhqYJzjvI_AVfhnxABX9T5sBX_OLPWkmSPvJAtxNTtDDS4nE6K1Ya4wRgzA-oG/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mkurugenzi-wa-jiji-arusha-atoa-semina.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mkurugenzi-wa-jiji-arusha-atoa-semina.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy