MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA WILAYA YA KATI UNGUJA

  Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Vion...


 Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi wa CCM Wilaya ya Kati na wa  Mkoa wa Kusini Unguja alipowasili  kwenye ofisi za CCM za Wilaya ya Kati.
 

Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa kamati za Siasa Tawi , wilaya na mkoa kwenye ukumbi wa TC Dunga, wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.

Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe 590 uliofanyika kwenye ukumbi wa TC Dunga , Mhe. Samia aliwataka wana CCM kukiimarisha chama katika mkoa wa Kusini Unguja , aliwaambia wajumbe hao kuwa CCMsi kadi CCM ni Itikadi, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha mafunzo ya itikadi mara baada ya chaguzi ndani ya chama kukamilika.

Alihimiza Vijana waambiwe mambo mazuri ya CCM  alisema  "CCM peke yake, ndio penye misingi,penye historia, na penye Malengo" na kutaka wananchi hao kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika kuleta maendeleo nchini.

Mhe. Samia pia alihimiza Makatibu kufanya kazi zao hasa katika kutoa taarifa sahihi za masuala ya uchaguzi badala ya kubeba watu na alizitaka Jumuiya kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni na utaratibu.

Aidha wakati wa kumkaribisha Mhe. Samia , Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdalla Juma Mabodi alisema Wazanzibar wapuuze porojo za wanasiasa waliopoteza muelekea kwani hata Jumuiya za Kimataifa zinaelewa CCM ndio inayotawala kwa mujibu wa Sheria na Katiba na aliahidi kufanya kazi zaidi na mashina.



 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdalla Juma Mabodi akihutubia kabla ya kumkaribisha Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa , Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye ukumbi wa TC Dunga wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
 BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA WILAYA YA KATI UNGUJA
MHE. SAMIA AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA KAMATI ZA SIASA WILAYA YA KATI UNGUJA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEvrgQII1-U7qMQEOwi2j8yiWZ33pfuZn_umytqWTK_WzUS85TTsczo3YmgQRiqjsvOTI2IUWXVCaiM3M4Nc0L9UYB2bh3jfDRZeuwtPeHVhP13goPbJAGJ9jTpweHecZ6hHZOJuQUGec/s640/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEvrgQII1-U7qMQEOwi2j8yiWZ33pfuZn_umytqWTK_WzUS85TTsczo3YmgQRiqjsvOTI2IUWXVCaiM3M4Nc0L9UYB2bh3jfDRZeuwtPeHVhP13goPbJAGJ9jTpweHecZ6hHZOJuQUGec/s72-c/2.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mhe-samia-azungumza-na-wajumbe-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/mhe-samia-azungumza-na-wajumbe-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy