MD KAYOMBO AKABIDHIWA MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI MSAKUZI
HomeJamii

MD KAYOMBO AKABIDHIWA MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI MSAKUZI

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza walimu juu ya utunzwaji wa madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi...

RC MAKONDA AWATAKA WAKUU WA WILAYA WOTE KUANZISHA KITENGO MAALUM CHA KISHERIA
TANZIA:TANGAZO LA KIFO CHA MZEE XAVERY MIZENGO PINDA
RAIS MAGUFULI ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA RAIS FIDEL CASTRO WA CUBA

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Ndg John Lipesi Kayombo akiwasisitiza walimu juu ya utunzwaji wa madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kuwasili shule ya Msingi Msakuzi katika dhifa ya makabidhiano ya madarasa
 Madarasa matatu ya shule ya Msingi Msakuzi yaliyokabidhiwa kwa MD Kayombo
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Ubungo walioshiriki kwenye dhifa ya makabidhiano ya madarasa ya shule ya Msingi Msakuzi

Na Nasri Bakari, Dar es salaam

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amekabidhiwa madarasa matatu yaliyokamilika na mkandarasi katika shule ya msingi Msakuzi.

Makabidhiano ya madarasa hayo ambapo ujenzi wake umegharimu shillingi millioni sitini na mbili (62 Mil) yamefanyika katika shule hiyo iliyopo katika Kata ya Mbezi Manispaa ya Ubungo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Kayombo amesema kuwa amefurahi kuona ujenzi wa madarasa hayo umemalizika kwa wakati na kutoa ahadi mbalimbali katika shule hiyo.

"Kwanza napenda nichukue fursa hii kukupongeza mkandarasi kwa kumaliza ujenzi ndani ya muda tuliokubaliana kwa hakika umeonyesha ni jinsi gani unajali kazi yako" Alisema MD Kayombo.

MD Kayombo amesema kuwa mpaka kufikia kesho tarehe 06/04/2017 madawati 120 yanapaswa kufikishwa kwenye shule hiyo huku akisema kuwa kila darasa yanapaswa kukaa madawati arobaini(40) kila chumba katika vyumba vitatu vya madarasa alivyokabidhiwa.

Pia ameahidi kuweka tarazo katika vyumba viwili vya madarasa ya zamani ambapo pia ameahidi kutoa mifuko Hamsini ya Saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ofisi ya walimu na kuahidi kuhakikisha shule hiyo inakuwa ya mfano.

"Fedha hizi za kununua mifuko ya Saruji nitatoa kwenye mshahara wangu hivyo namsihi Mheahimiwa Diwani wa eneo hili naye aweze kuchangia ujenzi huu" Alisema MD Kayombo
 "Tunakushukuru sana Mkurugenzi kwa jitihada ulizozionesha katika shule hii kwa kipindi kifupi kwa kutununulia eneo la shillingi Millioni 35 na kutujengea madarasa matatu mungu akubariki sana" Alisema Bi Shahiri.
Mkurugenzi Kayombo amewasihi walimu wa shule hiyo kujitahidi kutunza mali za serikali zikiwemo madarasa, madawati na samani nyingine.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MD KAYOMBO AKABIDHIWA MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI MSAKUZI
MD KAYOMBO AKABIDHIWA MADARASA MATATU SHULE YA MSINGI MSAKUZI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdjrHYUgnU3_Gx0dDSBe9wzuQ9KtrOvv1v1f0am7YDz7fzm-vSxQJ5BURrsbxOs-ivahJ_N_EqtArb1W-MCTiE1jMc_tIs4AF3WlPMQHBF4iKK1HlUtv2h9qQTVPpuJqyircDmbGx_s32b/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdjrHYUgnU3_Gx0dDSBe9wzuQ9KtrOvv1v1f0am7YDz7fzm-vSxQJ5BURrsbxOs-ivahJ_N_EqtArb1W-MCTiE1jMc_tIs4AF3WlPMQHBF4iKK1HlUtv2h9qQTVPpuJqyircDmbGx_s32b/s72-c/1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/04/md-kayombo-akabidhiwa-madarasa-matatu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/md-kayombo-akabidhiwa-madarasa-matatu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy