Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na m bunge wa Viti Maalum mkoa w...
Mbunge viti maalumu mkoa wa rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji

Mbunge viti maalumu mkoa wa Rukwa Bupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati (wa pili kushoto) akimkabidhi kiasi cha shilingi laki mbili kwa ajili ya
kununua mifuko ya saruji kwa ajili ya kukarabati shule ya Kigonzile
Na Fredy Mgunda,Iringa
Mbunge viti
maalumu mkoa wa rukwaBupe Mwakang'ata kupitia chama cha mapinduzi (CCM)
ameipiga jeki shule ya msingi Kigonzile iliyopo kata ya Nduli mkoani
iringa kwa kuipatia mifuko zaidi ya ishirini ya saruji kwa lengo la
kusaidia ukarabati wa shule hiyo akiwa na lengo la kumuunga mkono mbunge
wa Viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati katika juhudi za kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi saruji hiyo Mwakang'ata alisema kuwa ameamua kumuunga mkono mbunge huyo kwa kuwa ni mpenda maendeleo na mchapa kazi.
“Mimi
napenda kufanya kazi za kimaendeleo hasa za kijamii ndio maana kabati
aliponiambia kuwa anakuja kufanya maendeleo ya ukarabati wa shule ya
msingi kigozile nilikubali haraka kwa kuwa na napenda kufanya maendeleo”
alisema Mwakang'ata
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametutuma
kufanya kazi kwa wananchi wakawaida kwa kuwa wao ndio wanamahitaji mengi
kuliko watu wa kipato cha kati na cha juu hivyo hata mimi nimeamua
kufanya kazi za kwasaidia kuleta maendeleo wananchi wengi wa chini.
Aidha
Mwakang'ata aliwaomba wananchi na viongozi wa kufanya kazi kwa kujituma
ili kwenda sambamba na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Magufuli na kuomba jamii kufanya kazi za kujitolea zaidi kuliko
kusubili serikali kuleta maendeleo.
“Mkiwa
mnajitolea kama hii leo naamini tukiwa na wananchi na viongozi wengi
basi nchi hii itapata maendeleo ya haraka na kwa kasi kutokana na
wananchi kufanya kazi kwa nguvu na moyo wa kuinua uchumi”
alisema Mwakang'ata
Mwakang'ata
aliongeza kuwa shule nyingi za hapa nchi zilijengwa miaka mingi
iliyopita hivyo nyingi zimechakaa kutokana na kutokarabatiwa kwa wakati
hivyo nawaomba viongozi wengi kuwa wabunifu wakati wa kutafuta pesa
nyingi za kusaidia kukarabati miundombinu ya shule na maeneo mbalimbali
ilimradi kukuza uchumi na kutoa elimu bora.
“Hichi
nilichokitoa hii leo ni kidogo sana ila nimefurahishwa na kujituma
kwenu katika swala nzima la kusaidia ukarabati wa shule hii ya kigonzile
ambayo ilikuwa katika mazingira ya kufungwa kutokana na uchakavu wake”
alisema Mwakang'ata
Mwakang'ata
namkaribisha pia mbunge Ritta kabati kuja Rukwa pia aje asaidie
maendeleo kwa kuwa naye ni mpenda maendeleo na wananchi wa Rukwa
wanapenda maendeleo na ninahakika watampokea kutokana na uchapakazi
wake.
COMMENTS