Benjamin Sawe-Maelezo,Dodoma. MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa ametaka ujenzi wa makao m...
Benjamin Sawe-Maelezo,Dodoma.
MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk.
Albina Chuwa ametaka ujenzi wa makao makuu ya ofisi hiyo unaoendelea mjini
Dodom ukamilishwe kwa wakati.
Akizungumza mjini hapa jana baada ya kukagua ujenzi wa ofisi
hiyo, Dk. Chuwa alisema ni wakati sasa kwa NBS kuwa na ofisi yenye hadhi
kwa
ajili ya kuboresha na kuimarisha shughuli za takwimu nchini.Dk. Chuwa
alisema NBS ni miongoni mwa taasisi kongwe nchini na ambayo imekuwa
ikibadilika na kwenda na wakati hivyo kupatikana kwa jengo hilo ni jambo
linalopaswa kutimia haraka.
“Jengo letu ni la ghorofa tano tu, kwa kuwa mkandarasi
umepewa muda wa miezi 10 sioni sababu ya kuchelewa kukamilishwa.“Hivi karibuni nilizungumza na wenzetu wa Uganda wao
walijenga jengo lao la ghorofa 12 kwa mwaka mmoja tu sasa sioni sababu kwa nini
letu lisikamilike kwa wakati,”alisema.
Kwa mujibu wa Dk. Chuwa jengo hilo litakuwa ni la ghorofa
tano na kwamba kwa kuwa wanazo ofisi katika kila mkoa nchini, makao makuu hayo
yatatumika kuratibu uendeshaji wa shughuli za takwimu na mambo mengine ya
maendeleo yanayohusiana na NBS.
Dk. Chuwa alisema jengo hilo litagharimu sh. Bilioni 11.6
hadi kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa ujenzi huo, Mtumwa Shomvi
kutoka kampuni ya Y&P Achtects Limited, alisema watahakikisha wanatekeleza
majukumu yao kikamilifu katika kuusimamia mradi huo.Shomvi alisema jukumu kubwa wanalolisimamia ni kuhakikisha ujenzi huo
unakamilika kwa wakati, gharama na ubora uliokubaliwa.
Aidha, Msimamizi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya
Hainani International Limited ya China, Lan Shuiqing alisema kazi ya ujenzi
inaendelea vyema na kwamba anaamini kila kitu kitakamilika kwa wakati.
Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kwanza kulia ni Injinia Lan Shuiqing kutoka Kampuni ya Hainan Internationa.

Msimamizi Mkuu kutoka Kampuni ya Y and P Bw. Mtumwa Somvi wa kwanza kulia akitoa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa wakati menejimenti ya Taasisi hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi mkoani Dodoma leo (jana).

Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu lenye urefu wa ghorofa tano linaloendelea kujengwa Mkoani Dodoma.

Muonekano wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu unavyoendelea mkoani Dodoma.(Picha na Benjamin Sawe -Maelezo) .
COMMENTS