WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUFUNGUA MKUTANO WA TISA WA WADAU WA LAPF JIJINI ARUSHA

  Meneja  Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (katikati), akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu mku...



 Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe (katikati), akizungumza katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa tisa wa LAPF utakaofanyika Machi 9 na 10, 2017 Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Kulia ni Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata na Ofisa Masoko na Mawasiliano wa LAPF, Rehema Mkamba.


 Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Kushoto ni Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Wapiga picha wakichukua taarifa hiyo.

Dotto Mwaibale na Christina Mseja

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kufungua mkutano wa tisa wa wadau wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF jijini Arusha.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo,  Meneja Masoko la Mawasiliano wa LAPF, James Mlowe alisema mkutano huo utafanyika kwa siku mbili Machi tisa na 10 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha.

Alisema lengo la mkutano huo ni kutoa za uendeshaji wa Mfuko na kuwapa fursa wadau kutoa maoni yao mbalimbali ili kuboresha utendaji wa mfuko.

"Mikutano hii hufanyika ili kutekeleza maagizo ya mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii nchini (SSRA) " alisema Mlowe.

Alisema kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "Kuibua Fursa Endelevu za Ajira kwa maendeleo ya Jamii Tanzania"

Aliongeza kuwa pamoja na mambo mengine kwenye mkutano huo mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo mada inayohusu kauli mbiu iliyotajwa.

Mada nyingine zitahusu utendaji wa mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na taarifa ya uwekeza pamoja na taarifa ya Hesabu za Mfuko kwa mwaka 2015/2016.

Alisema siku ya kwanza ya ufunguzi wa mkutano  LAPF itazindua  huduma ya mkopo wa kujikimu ijulikanayo kwa jina la Maisha popote na LAPF kwa kushirikiana na benki ya CRDB .

"Huduma hii imewanufaisha  sana wanachama wa mfuko wanaonza ajira kwa kuwapa fursa ya kukopa mara tatu ya mshahara wao kukidhi mahitaji ya awali kama kulipa pango,nk kwa riba nafuu" 

Aliongeza kuwa  ufunguzi wa mkutano huo tarehe 9 machi,2017 itakuwa siku ya maadhimmishi ya figo duniani hivyo LAPF itatumia siku hiyo kuwapa fursa  wadau wote watakao shiriki mkutano huu kupima figo  kwa kushirikiana na watalaamu kutoka Hopstali ya KCMC.

LAPF inatarajia kupata washiriki zaidi ya 600 katika mkutano huu kwa kuzingatia idadi ya waalikwa. 

Meneja wa Takwimu Hadhari na Tathmini wa LAPF, Abubakar Ndwata alisema kwa mwaka wa fedha wa 2015-2016  mafao yaliokusanywa ni  sh. bilioni 107.25 na sh. bilion 2 kwa ajili ya mafao ya uzazi.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUFUNGUA MKUTANO WA TISA WA WADAU WA LAPF JIJINI ARUSHA
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUFUNGUA MKUTANO WA TISA WA WADAU WA LAPF JIJINI ARUSHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPKFQIH2caKS8HEkhADKsoyJl2hbRLQMqeN84JxZgANHBHdxs9lQhqB9oFXBLTTm2VrKWcCeAB8bI52badgaG_8YAj-u82wAQdSY6hpOUo74FBR5f4SQgRZTrYZXiKmeFXszI2qbaSLlMz/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPKFQIH2caKS8HEkhADKsoyJl2hbRLQMqeN84JxZgANHBHdxs9lQhqB9oFXBLTTm2VrKWcCeAB8bI52badgaG_8YAj-u82wAQdSY6hpOUo74FBR5f4SQgRZTrYZXiKmeFXszI2qbaSLlMz/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mkuu-kassim-majariwa-kufungua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/waziri-mkuu-kassim-majariwa-kufungua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy