Askofu wa Kanisa la Good news Ministry Dk. Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli...

Askofu wa Kanisa la Good news Ministry Dk. Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumpongeza Rais Dk. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es Salaam.
Askofu wa Kanisa la Good news Ministry Dk. Charles Gadi amempongeza Rais Dk. Jonh Pombe Magufuli kwa hatua yakuzuia mchanga uliokuwa wanataka kusafirisha nje ya nchi ili kuweza kuchakata dhahabu.
Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam Askofu Gadi amesema kuwa kusafirisha mchanga wa`madini ya dhahabu ni sawa na kuiuza Tanzania nje ya nchi.
Amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa mtu wa kuthubutu kuona nchi ya Tanzania inakuwa ya maendeleo na wananchi baada wataona mafanikio hayo.
Gadi amesema kuwa wakiwa viongozi wa dini wanajibu wa kumuombea Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ifanikiwe kutokana na harakati zake. Aidha wa amesema kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana kutokana na Rais kuweka kipaumbele kwa wawekezaji ili Tanzania kuingia katika rekodi ya uchumi wa kati.
COMMENTS