Mbunge wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. (Picha...
Mbunge
wa jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na madiwani wa
halmashauri hiyo katika baraza la madiwani. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Mbunge
wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete pamoja na madiwani wa
halmashauri ya Chalinze ,wameujia juu uongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira Chalinze CHALIWASA kwa kushindwa kusambaza maji ili
kuondoa kero hiyo .
Amesema
mradi huo ulitakiwa kukabidhiwa mwezi huu jimboni hapo lakini
unasuasua.Ridhiwani aliyasema hayo kwenye baraza la Madiwani
lililofanyika Lugoba.Alisema tatizo la ukosefu wa maji, bado ni kubwa
hivyo inaonekana uongozi wa Mamlaka hiyo umeshindwa kutatua.
Ridhiwani
alifafanua kwamba hadi sasa hakuna matenki yaliyojengwa na mabomba
hayajafukiwa hivyo ni ndoto za alinacha mradi huo kukamilika mwezi
huu.Kwa mujibu wake, waziri wa maji anapaswa kulieleza bunge na wananchi
wa Chalinze fedha za maji zilizopelekwa kwa ajili ya mradi huo na mwezi
wa kuumaliza .
"Kama
mradi huu utaendelea kusuasua wananchi na wawekezaji wanaokimbilia
kuwekeza Chalinze watashindwa kutimiza malengo yao na kuendelea kuishi
kwenye adha hii inayowapa wakati mgumu "alisema Ridhiwani.Nao madiwani
walisema, kama uongozi wa mamlaka hiyo umeshindwa kazi basi wawapishe
.Diwani wa Lugoba, Rehema Mwene,aliiomba serikali imsimamie mjenzi wa
mabomba na matenki amalize kazi hiyo.
Nae
Hassan Mwinyikondo, alieleza hatari kubwa kwa wananchi wa maeneo ya
Bwilingu na Chalinze ambao wanatumia maji yasiyo safi wala salama.
Alisema mradi wa maji wa CHALIWASA hauna faida, kutokana na wananchi kukosa maji kwa kipindi kirefu.
Hussein
Hading'oka aliweka hofu katika kipindi kinachokuja kuwa cha mvua za
masika na kuongeza kwamba mara kadhaa viongozi wa CHALIWASA wamekuwa
wakisema kipindi cha mvua mitambo yao huwa inasumbuliwa na tope.hivyo
kushindwa kufanyakazi za kusukuma maji.
Alimshangaa
Meneja wa Mamlaka hiyo Mhandisi Christer Mchomba kushindwa kuhudhuria
kikao hicho kama alivyotakiwa na Mkurugenzi Edes Lukoa .
Meneja
huyo alitakiwa kwa ajili ya kuwapatia Madiwani hao maelezo ya kina
kuhusiana na tatizo sugu la maji linalowakabili wananchi wa Halmashauri
hiyo kwa miaka mingi sasa.Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Edes Lukoa
alisema Halmashauri imetenga bajeti iwa ajili ya maeneo ambayo
hayafikiwi na CHALIWASA hivyo mamlaka hiyo lazima iwe na mpango wake.
Hivi
karibuni Waziri wa Mazingira Januari Makamba alipofanya ziara ndani ya
Halmashauri hiyo alifika eneo la chanzo cha maji Wami na kutoa maagizo
kwa wilaya na mkoa.Aliagiza Mkuu wa wilaya Alhaj Hemed Mwanga
kuhakikisha na Mkoa wanakutana na wenzao wa Morogoro kuzungumzia suala
la wafugaji wanaotokea Morogoro kuvamia kando ya mto WAMI na kuhakikisha
wakulima wanaolima kando ya mto wondolewe mara moja.
COMMENTS