WAZIRI MKUU AAGIZA UMEME WA UHAKIKA KISARAWE II
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kitanda wakati alipotembelea wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni ya mafuta ya OILCOM katika  ENEO la  Kisarawe Two wilayani Kigamboni, Januari 4, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa.
HomeJamii

WAZIRI MKUU AAGIZA UMEME WA UHAKIKA KISARAWE II

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II ...

ZAINA FOUNDATION HELP WOMEN TO ICREASE KNOWLEDGE IN CYBER SECURITY
WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WABUNGE WANAOTOKA MIKOA INAYOLIMA PAMBA
SERIKALI YAREJESHA UMILIKI HALALI WA KIWANJA KILICHOUZWA KWA HATI ZA KUGHUSHI







WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhakikisha eneo la Kisarawe II linakuwa na umeme wa uhakika ili kuwezesha viwanda na wananchi wa eneo hilo kupata nishati hiyo.



Alitoa agizo hilo jana jioni (Jumanne, Januari 3, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha Milkcom kinachozalisha bidhaa za maziwa na kiwanda cha Watercom kinachozalisha maji vilivyoko katika kata ya Kisarawe ii wilayani Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.



“Waziri wa Nishati ahakikishe eneo hili linapata umeme wa uhakika ili kuviwezesha viwanda hivi kufanyakazi vizuri jambo litakaloongeza uzalishaji. Pia wananchi wanaoishi katika maeneo haya nao watanufaika na upatikanaji wa nishati hiyo,” alisema.



Waziri Mkuu alisema amefarijika na jitihada za muwekezaji huyo za kuungamkono mkakati wa Serikali ya awamu ya Tano wa kuifanya Tanzania kujenga uchumi wa viwanda utakaoliwezesha Taifa kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.



Awali, Msemaji wa Viwanda hivyo, Aboubakar Faraj akisoma taarifa ya viwanda hivyo kwa Waziri Mkuu alisema moja ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika jambo linasababisha kupanda kwa gharama za uzalishaji.



“Punde umeme unapokatika tunalazimika kutumia majenereta kwa muda mrefu. Hii husababisha ongezeko la gharama za uzalishaji ambazo huumiza kiwanda kwa sababu haiwezekani kumtwisha mzigo huu mlaji,” alisema.



Faraji alisema changamoto nyingine ni miundombinu ya barabara ambayo usababisha wateja wengi kushindwa kufika kwenye viwanda hivyo kwa urahisi, hivyo aliiomba Serikali kuwatatulia kero hilo.



Aliongeza kuwa kwa sasa viwanda hivyo vimeajiri watu zaidi ya 1,800, ambapo alisema endapo Serikali itawahakikishia upatikanaji wa umeme na barabara wataongeza ajira kwa asilimia 25 ifikapo mwaka 2018.



Mapema Waziri Mkuu alizindua wodi ya wazazi katika Zahanati ya Kisarawe ii iliyojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya mafuta ya Oilcom. Wodi hiyo yenye vyumba vitatu itawapunguzia akinamama kusafiri umbali mrefu kutuata huduma hiyo.





 IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

S.  L. P. 3021,

JUMATANO, JANUARI 4, 2017







Wananchi wa eneo la Kisarawe Two wilayani Kigamboni wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao baada ya kukagua wodi ya wazazi iliyojengwa na kampuni ya mafuta ya OILCOM kijijini hapo. Waziri Mkuu alikuwa katika ziara ya wilaya hiyo Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngombe wa kisasa wakati alipotembelea  shamba la ng'ombe wa maziwa  la MILKCOM  TANZANIA LIMITED  lililopo Kigamboni  jijini Dar es Salaam. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngombe wa kisasa wakati alipotembelea  shamba la ng'ombe wa maziwa  la MILKCOM  TANZANIA LIMITED  lililopo Kigamboni  jijini Dar es Salaam. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngombe wa kisasa wakati alipotembelea shamba la ng'ombe wa maziwa  la MILKCOM  TANZANIA LIMITED  lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam. Alikuwa katika ziara ya wilaya ya Kigamboni Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi wakati alipotembelea  maghala ya NFRA, Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017. Kulia kwake ni  Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua mahindi wakati alipotembelea magahala ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Chang'ombe jijini Dar es salaam Januari 4, 2017. Kulia kwake ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Deusdedit Mpazi wakati alipotembelea  maghala ya NFRA, Chang'ombe jijini Dar es Salaam Januari 4, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU AAGIZA UMEME WA UHAKIKA KISARAWE II
WAZIRI MKUU AAGIZA UMEME WA UHAKIKA KISARAWE II
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihd6kePHzm0GyVBYWyyvGxYDhd7Zoaacmmf9cf9IkZXlGvj4ztRIcxMWfi_soyy1VpFTInnZ3A4Q86W98ZtHyo_jGJF9d0lul46Ncfpzp_ijH-IiIjVERxf7WOhiSxkWQev_tTZxqjf7U/s640/IMGM0015.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihd6kePHzm0GyVBYWyyvGxYDhd7Zoaacmmf9cf9IkZXlGvj4ztRIcxMWfi_soyy1VpFTInnZ3A4Q86W98ZtHyo_jGJF9d0lul46Ncfpzp_ijH-IiIjVERxf7WOhiSxkWQev_tTZxqjf7U/s72-c/IMGM0015.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/waziri-mkuu-aagiza-umeme-wa-uhakika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/waziri-mkuu-aagiza-umeme-wa-uhakika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy