Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali, wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa jiji la ...
Mkuu
wa Mkoa Paul Makonda akizungumza mbele ya wageni waalikwa
mbalimbali, wakiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa jiji la
Dar,viongozi wa Dini mbalimbali, Wasaniii na vijana kutoka vituo
mbalimbali vya matibabu ya dawa za kulevya walijitokeza kumsikiliza RC
Paul Makonda ambaye leo alikuwa anatimiza mwaka wake mmoja wa Uongozi
tangu aapishwe na Rais wa awamu ya tano, Dkt John Pombe Magufuli.
Baadhi
ya waathirika wa Madawa ya Kulevya wapato zaidi ya 1500 kutoka vituo mbalimbali vinavyotoa
matibabu ya Dawa za kulevya,wakiwa ndani ya bwalo la Polisi Oysterbay
jijini Dar,wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alipokuwa akizungumza
nao mambo mbalimbali,ya kimaendeleo pamoja na kupewa elimu mbalimbali
ihusuyo dawa za kulevya.RC Makonda leo anatimiza mwaka mmoja tangu
aapishwe kuwa mkuu wa mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,
Baadhi
ya Viongozi mbalimbali wa dini,walialikwa kwenye hafla hiyo fupi ya
kutimiza mwaka mmoja kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar,Paul Makonda
Pichani
ni baadhi ya wasanii walioshiriki na kutoa neno katika hafla
hiyo,wasanii hao ni TID,Diamond Paltnumz,Harmonize,Banana Zorro,Mrisho
Mpoto na wengineo ambao walijitokeza kumuunga mkono RC Makonda katika
suala zima la kupambana na Dawa
za kulevya.
Vijana
waliothiriwa na Madawa ya kulevya ambao kwa sasa wameahidi kuacha
kutumia wakiwa wameandika bango lao la kumshukuru RC Makonda kwa kazi
yake nzuri aifanyayo ya kupambana na Dawa za Kulevya.
Vijana
mbalimbali walikokuwa wakitumia dawa za kulevya wakimshukuru RC Makonda
kwa juhudi zake kubwa za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokea ndani ya
jiji la Dar kwa namna moja ama nyingine
COMMENTS