RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agizo lililotolewa jana na Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Wananchi wanaohitaji kufunga ndoa kuanzia mwezi Mei mwaka huu kuwa na vyeti vya kuzaliwa. Rais Mhe. Dkt. Magufuli ameagiza utaratibu wa awali uendelee kutumika kwasababu wananchi wengi wa Tanzania hawana vyeti, hivyo wangekosa haki hiyo ya kufunga ndoa. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana.
HomeJamii

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanahabari Mkoani Dodoma kuhusiana na kufuta agiz...

HALI YA USALAMA BARABARANI YAIMARIKA:KAMANDA MUSILIMU
MAVUNDE AJIBU KERO ZA WANANCHI WA HOMBOLO
VIONGOZI WA UMMA WAKUMBUSHWA KUWASILISHA FOMU ZA TAMKO LA RASILIMALI ZAO




(PICHA NA IKULU)
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amelifuta agizo lililotolewa jana tarehe 16 Machi, 2017 na Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe linalotoa sharti la kuwa na cheti cha kuzaliwa kwa watu wote watakaofunga ndoa kuanzia tarehe 01 Mei, 2017.
Mhe. Rais Magufuli amefuta agizo hilo leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari muda mfupi kabla ya kuondoka katika Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma na kurejea Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dkt. Magufuli amesema Serikali haiwezi kuruhusu sharti hilo kutumika kwa kuwa litawanyima haki ya kuoa na kuolewa Watanzania wengi ambao hawana vyeti vya kuzaliwa, huku utaratibu wa kupata vyeti hivyo ukiwa bado unakabiliwa na changamoto nyingi kwa wanaohitaji.
Amesema mpaka sasa idadi ya Watanzania walio na vyeti vya kuzaliwa ni chini ya asilimia 20 huku wengi wao wakiwa ni wananchi waishio vijijini ambako ni vigumu kupata vyeti hivyo, na wengine wakiwa ni waliozaliwa kabla ya kuanza kutolewa kwa vyeti vya kuzaliwa nchini mwaka 1961.
“Kwa hiyo ndugu zangu Watanzania msiwe na wasiwasi wowote, endeleeni na utaratibu wenu wa kuoa na kuolewa kama kawaida na kama kuna kifungu chochote cha sheria kinachomlazimisha mtu awe na cheti cha kuzaliwa ndipo aoe ama aolewe nitamuelekeza Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Harrison Mwakyembe apeleke Bungeni kikarekebishwe” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa wanasheria kuziangalia vizuri sheria zinazohusiana na kuzaliwa na kifo na kuoa na kuolewa ili zisilete mkanganyiko kwa wananchi.
Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kupata vyeti vyao vya kuzaliwa kama kawaida na amewataka viongozi wote kuwahamasisha wananchi kuwa na vyeti hivyo.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Chamwino
17 Machi, 2017





Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA
RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFUTA AGIZO LA KUFUNGA NDOA KWA SHARTI LA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA
https://i.ytimg.com/vi/1_hJDgGnoRo/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/1_hJDgGnoRo/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/03/rais-mhe-dkt-magufuli-afuta-agizo-la.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/rais-mhe-dkt-magufuli-afuta-agizo-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy