Naibu Waziri Mpina (katikati) akiwa na ujumbe wake, akisisita jambo wakati wa ukaguzi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko kati...
Naibu
Waziri Mpina (katikati) akiwa na ujumbe wake, akisisita jambo wakati wa
ukaguzi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika Delta ya Rufiji Kaskazini.
Naibu
Waziri Mpina (katikati) na Ujumbe wake katika picha wakitembea kukagua
mikoko iliyopandwa katika Delta ya Kaskazini Rufiji.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina
na ujumbe wake wakiwa katika boti wakielekea katika ukaguzi wa upandaji
na utunzaji wa Mikoko, pamoja na uharibifu wa Mazingira katika Delta ya
Rufiji Kaskazini.

Naibu
Waziri Mpina akiwaasa wasimamizi wa mradi wa upandaji na utunzaji
mikoko katika delta ya Kaskazini Rufiji hawapo pichani wamueleze ukweli
kuhusu matumizi ya fedha na hali halisiya mradi kabla ya kwenda kukagua
upandaji, utunzaji wa mikoko na uharibifu wa mazingira.
NA EVELYN MKOKOI -RUFIJI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 396 za ufadhili wa Mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia mabadiliko ya tabianchi katika utekelezaji wa mradi wa upandaji na uendelezaji wa mikokokatika delta ya kaskazi mto Rufiji.
Katika mradi huo matumizi ya zaidi ya sh. milioni 364 mchanganuo wake
hauridhishi huku vikundi vinavyodaiwa kulipwa fedha hizo vikikana kulipwa na kusema hawakuwa na mkataba bali walifanya kazi kama vibarua kwa posho ya sh. 10000 kila wanapomaliza kazi na hawakuwa na mkataba.
Kutokana
na hatua hiyo Mpina amemuagiza Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mwatano Maganga kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja anafanya uhakiki
wa matumizi ya fedha hizo za mradi na kuelekeza hatua za kuchukua
kwakuwa.
vielelezo alivyokabidhiwa na Msimamizi wa mradi kutoka Halmashauri ya
Rufiji
Sabastian Gaganijas vina mashaka. “Naagiza ukaguzi ufanyike, lazima
kuna ubadhilifu umefanyika katika utekelezaji wa mradi, baada ya ukaguzi
makini, tutajua ukweli na kubaini hatua gani zitachukuliwa.”
Alisisitiza Mpina.
1000 zilizodaiwa zimepandwa ni udanganyifu wa wazi.
Hata hivyo, baada ya zoezi zima la kukagua Delta hiyo yenye kilomota zaidi ya 5
Naibu Waziri Mpina, alisema amesikitishwa na jutekelezaji wa mradi huo
unaotumia fedha za wafadhili zaidi ya sh.milioni 396 kuwa na madudu na
amejionea mwenyewe kuwa, mradi hauna usimamizi na kusema kuwa, kuna dalili ya fedha hizo kutumika ndivyo sivyo kwakuwa hata hekta 792 kati ya
“Huu ni uhuni ambao haukubali kwa serikali hii awamu ya tano tuliposema
hapa kazi tu tulimaanisha kuwa hatuwezi kudanganywa watu wamezoea kuona Waziri hawezi kuja kwenye mazingira kama haya nimejionea mwenyewe mikoko iliyopandwa haendani na thamani ya matumizi ya fedha hizo na sehemu kubwa imevamiwa na kupandwa mpunga badala ya mikoko,”alisema.
Alisema katika mchanganuo aliokabidhi na msimamizo wa mradi fedha hizo
zaidi ya sh.milioni 364 zimedaiwa matumizi yake ni pamoja na kulipa
vikundi 28 vilivyokabidhiwa mradi ambavyo sasa havipo.
Alisema cha kushangaza katika fedha hizo kipo kikundi kimelipwa zaidi ya
milioni 30 kwa kupanda hekta 3 huku kingine kikilipwa milioni 3 kwa hekta
hizo hizo.
Baadhi
ya wakazi wa rufiji wakizungumza katika ziara ya Naibu Waziri Mpina,
wametoa changamoto zao katika kukabiliana na uharibifu huo wa Mazingira
na kuiomba Serikali kuongeza usimamizi madhubuti katika mradi huo ili
kukubaliana na uharibifu huo wa hifadhi hiyo ya mikoko,
Awali
Imeelezwa na mtaalam wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Cretus Shengena kuwa, uharibifu huo waMikoko unaweza kusababisha kupotea
kwa uoto asili na baiyonuwai katika eneo hilo kama udhibiti wa dhati
usipo chukuliwa kwa haraka kuinusuru eneo hilo la Delta ya Rufiji
kaskazini.
Mradi
huo wa hifadhi ya taifa ya Delta ya Rufiji kaskazini unafadhiliwa na
Mfuko wa kundi la nchi maskini zaidi duniani (LDCF) kupitia Shirika la
umoja wa Mataifa ya Mazingira chini ya usimamizi wa Ofisi ya Makamu wa
Rais.
COMMENTS