Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafungua tena kazi za uchimbaji mcha...
Alisema
maamuzi hayo ya Serikali yatakwenda sambamba na utolewaji wa bei
elekezi ya mchanga ili kujaribu kuzuia uharibifu wa mazingira
uliokwishaathiri maeneo mengi yaliyokwishachimbwa mchanga pamoja
naulanguzi wa kupita kiasi kwa wauzaji wa rasilmali hiyo.
Akitoa
Hoja ya kuahirisha Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi
Zanzibar huko Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Wizara ya Kilimo itaandaa zamu za kuchimba mchanga ili
kupunguza msongamano wa gari zitakazokwenda katika maeneo ya Mchanga.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi Akitoa Hoja ya kuahirisha
Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar huko Mbweni
Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema
zamu hizo zitawapa fursa ya siku Tatu kwa Wiki Wananchi wa kawaida
kupata rasilmali hiyo ya Mchanga na Siku Mbili kwa Wiki zitazingatiwa
kwa Makampuni na Taasisi za Serikali zilizopata vibali vya Ujenzi
wakati Jumamosi na Jumapili zitakuwa siku za mapumziko.
Balozi
Seif alisema utafiti unaendelea kufanywa na Kamati ya Wataalamu kwa
kushirikiana na ile ya Mawaziri inayoshughulikia suala mchanga kujua
kiwango cha mchanga kiliopo kwenye eneo la Kiwanda cha Sukari Pangatupu,
Kichwele na maeneo mengi ili kubaini wingi wake na endapo utafaa kwa
matumizi ya ujenzi.
Alisema
Zanzibar si nchi ya kwanza kuwa na upungufu wa mchanga ambapo ipo
mifano ya uhaba wa rasilmali hiyo iliyokwishajitokeza katika baadhi ya
nchi duniani kama vile Malaysia, Singapore, Phillipines na Tuvalu.
Balozi
Seif alieleza kwamba upo ushahidi wa wazi uliothibitisha kuzama kwa
Visiwa vodogo vidogo Vitano Nchini Phillipines kufuatia wimbi kubwa la
uchimbaji wa mchanga kiholela pembezoni mwa fukwe zilizokuwa
zimevizunguuka Visiwa hivyo.
Alifahamisha
kwamba ushibiti huo wa rasilmali ya mchanga unaweza kupelekea Wananchi
katika maeneo mbali mbali Nchini wakavamia fukwe kuchota mchanga. Hivyo
aliziomba mamlaka zote kupiga marufuku uchotaji huo ili kujiepusha na
majanga na kuangamiza Visiwa hivi.
Alitahadharisha
kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia vyombo vyake itatoa
adhabu kali kwa mtu ye yote atakayekwenda kinyume dhidi ya agizo
lililotolewa na Serikali kuhusu suala zima la uchimbaji wa mchanga.
Wajumbe
wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kuahirishwa
kwa Mkutano wa Tano wa Baraza la Tisa la Wawakilishi Zanzibar
iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
hayupo pichani. (Picha na – OMPR – ZNZ)
Akizungumzia
vita dhidi ya Dawa za kulevya vilivyotangazwa hivi karibuni na Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alionya kwamba Zanzibar haitakua
kimbilio la waendelezaji wa biashara hiyo haramu na badala yake itakuwa
gereza lao.
Balozi
Seif alisema vita hivyo ni vya Nchi nzima ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania ikiwemo Zanzibar. Hivyo wale wanaofikiria kwamba vita hivyo ni
kwa Tanzania Bara pekee wanaelezwa bayana kuwa wamepotea njia.
Alisema
Takwimu kutoka Tume ya Uratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya
zinaonyesha kwamba mwaka 2016 jumla ya kesi 37 ziliripotiwa kwenye
Mahakama za Unguja na Pemba na ni Mtu Mmoja tu ndie aliyetiwa hatiani.
Akigusia
vita dhidi ya ukatili na udhalilishaji wa kijinsia hasa kwa wanawake na
watoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema bado lipo ongezeko
kubwa la vitendo hivyo vinavyoshinda kutoa matunda mazuri
yaliyokusudiwa.
Alisema
takwimu za vitendo hivyo viovu zilizoripotiwa kuanzia mwezi Julai hadi
Septemba Mwaka 2016 zinazonyesha jumla ya matukio 218 yamewasilishwa
katika vyombo vinavyohusika Unguja na Pemba.
Balozi
Seif alitahadharisha kwamba hali hiyo bado inatisha na kutoa ujumbe
kuwa bado Jamii inahitaji kushirikiana kwa karibu kujaribu kutokomeza
vitendo vya udhalilishaji vya Kijinsia hapa Nchini.
Baraza la Wawakilishi Zanzibar limeahirishwa hadi Jumatano ya Tareje 10 Mwezi Mei mwaka 2017.




COMMENTS