Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge y...
- Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Prof. Norman Sigala na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu (kushoto).
- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL, Mhandisi Omar Nundu (kulia) alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea TTCL.
- Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (kushoto) akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL kwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea TTCL.
Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeitaka Taasisi za Serikali na
Mashirika yote ya Umma kutumia kituo cha kutunzia kumbukumbu cha Taifa
(National Data Centre)chenye hadhi ya juu kabisa katika viwango vya
ubora na usalama wa Taarifa na Kumbukumbu. Kamati pia imezitaka Taasisi
zote zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutumia
Kituo hicho katika kutunza kumbukumbu zake ili kuwa mfano kwa Taasisi
nyingine za Umma.
Akizungumza
katiko maazimio ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mara baada
ya ziara ya siku moja ya Kamati hiyo kuitembelea Kampuni ya Simu
Tanzania TTCL pamoja na miradi ya Mkongo wa Taifa na Kituo Mahiri cha
kutunzia kumbukumbu (Data Centre), Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa
Norman Sigala amesema, uhai wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL upo
mikononi mwa Serikali ambayo ina jukumu kubwa la kuihusiha Kampuni hiyo
yenye uwekezaji mkubwa.
Aidha,
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imezitaka Taasisi zote za Umma
na binafsi kulipa madeni zinazodaiwa na TTCL kuiwezesha Kampuni hiyo
kujiendesha kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na Watendaji wa Umma
wanaogharamiwa huduma za Mawasiliano kutumia huduma za simu za TTCL
katika maeneo yote yenye huduma hizo.
Mjumbe
wa Kamati hiyo Mhe Rita Kabati amesema, kukamilika kwa Mchakato wa
kuondoka kwa Bharti Airtel ndani ya TTCL kunahitaji kwenda sambamba na
uwezeshaji wa mtaji kama ilivyofanyika kwa Kampuni ya Reli Tanzania(TRL)
na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambazo sasa zinafanya vizuri.
- Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano), Mhandisi Dk. Marry Sassabo akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya maswali yalioulizwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kampuni ya TTCL.
- Meneja Mtandao wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Amani Kichele (wa pili kulia mwenye shati jeupe) akitoa maelezo kuhusu masuala mbalimbali ya Mkongo wa Taifa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu walipotembelea kampuni ya TTCL leo jijini Dar es Salaam.
Awali
akizungumza katika kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw
Waziri Kindamba amesema, ushirikiano mkubwa uliotolewa na Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Miundombinu umewezesha Serikali kuchukua hatua ambazo
zimeipa TTCL nguvu mpya ya kurejea katika nafasi yake ya kihistoria ya
kuwa Kinara wa utoaji huduma za Mawasiliao nchini.
Miongoni
mwa hatua hizo ni pamoja na Serikali kulipa sh Bilioni 14.7 na
kuhitimisha ubia usioridhisha wa Kampuni ya Bharti Airtel ndani ya TTCL
uliodumu kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu bila kuleta tija
iliyotarajiwa. Hatua nyingine ni pamoja na Serikali kuiruhusu TTCL
kutumia majengo yake kama dhamana kuweza kupata mikopo ya Shilingi
bilioni 96.6 kwa ajili ya uwekezaji, kurekebisha mizania ya Kampuni kwa
kufuta madeni ya takribani Shilingi bilioni 100 hivyo kufanya Kampuni
kuweza kukopesheka.
Maamuzi
mengine ni Serikali kuipatia TTCL masafa ya Megahezi 1800 na 2100
ambayo yametumika kufunga mitambo ya mawasiliano ya teknolojia za 2G
(GSM), 3G (UMTS) na 4G (LTE) pamoja na kuikabidhi TTCL dhamana ya
kusimamia na kuendesha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano(NICTBB) na Kituo
cha Kimataifa cha kuhifadhia kumbukumbu za kimtandao (National Internet
Data Centre).
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Mheshimiwa Omari Nundu amesema,
TTCL inakabiliana na changamoto kadhaa zinazohitaji utatuzi wa haraka.
Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na TTCL kukosa mtaji wa
kutosha( Takriban shilingi bilioni 300) kunununua teknolojia za kisasa
na mitambo mipya ili kuondoa miundombinu chakavu na kuongeza ufanisi na
ubora wa huduma.
Changamoto
nyingine ni madeni ya ankara za huduma ambayo TTCL inadai taasisi za
Umma na serikali ambayo yamefikia takribani Sh Bilioni 9 ambazo endapo
zingelipwa kwa wakati, zingesaidia sana kuimarisha utendaji wa TTCL.
Nao
Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja Mhe Japhari Michael na Mhe Prof
Anna Tibaijuka wamesema, TTCL inao wajibu mkubwa kwa Taifa kuhakikisha
kuwa Mawasiliano yanafika nchi nzima na hasa katika maeneo ya Vijijini
ambako Kampuni binafsi za Mawasiliano hazitoi kipaumbele katika
kufikisha huduma zake.
- Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
- Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
- Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakimsikiliza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Kindamba (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada juu ya miradi ya Serikali ambayo inasimamiwa na TTCL leo jijini Dar es Salaam.
COMMENTS