Mkuu wa wilaya wa Kinondoni Ally Hapi, akitoa taarifa ya ubadhilifu wa fedha katika mradi wa TASAF wilaya ...
Mkuu
wa wilaya wa Kinondoni Ally Hapi, akitoa taarifa ya
ubadhilifu wa fedha katika mradi wa TASAF wilaya ya Kinondoni na
kuamrisha Mratibu wa wilaya hiyo kusimamishwa kazi ili kupisha
uchunguzi, kushoto ni Naibu mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni Dennis Manumbu na kulia ni OCD wa
Kituo cha Polisi Magomeni.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MKUU
wa Wilaya Ya Kinondoni Ally Hapi amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri
Ya Wilaya ya Kinondoni Kumsimamisha kazi Mratibu wa mradi wa TASAF wa
wilaya hiyo Onesmo Onyango kutokana na ubadhilifu wa fedha za serikali
kwa kuwapatia kaya ambazo hazikustahili kupewa.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kutoa maagizo hayo, DC Hapi amesema
kuwa mratibu huyo alitoa fedha taslimu kiasi cha milioni 266 kwa kaya
537 ambazo hazijulikani makazi yake na milioni 180 kwa kaya 517 ambazo
hazistahili kupewa kutokana na kutokuwa na vigezo ikiwemo kuwa na uwezo
wa kujikimu kimaisha na wengine ni wafanyakazi wa serikalini.
Hapi
amesema, jumla ya kaya 1397 hawana sifa za kupatiwa fedha hizo za mradi
wa TASAF ambazo ni mali ya serikali na zaidi inawataka TASAF kuchukua
hatua kali za kisheria kwa wale ambao hawakuwa na vigezo pamoja na
kuzitaka kaya hizo kurudisha fedha zote walizozichukua katika vipindi saba tofauti.
"Kama
kutakuwa na njia zozote za rushwa na udanganyifu wowote katika utoaji
wa fedha hizi kwa kaya ambazo hazina vigezo na zingine hazijulikani
zilipo, basi jeshi la usalama la Polisi na Taasisi ya kuzuia na
kupambana na Rushwa zihusike mara moja kwa kuwakamata wahusika
waliofanikisha ubadhilifu huo kuanzia kwa Mwenyekiti wa serikali za
mitaa kwani yeye ndo wa kwanza anayewajua wakazi wake,"amesema Hapi.
Hapi
amesema kuwa mbali na kaya ambazo hazikustahili kupatiwa fedha hizo,
zipo zingine ambazo zinastahili ingawa hazijulikani zilipo na nyingine
zimehama kutoka wilaya ya Kinondoni.
Hayo
yamegundulika baada ya Mkuu huyo wa wilaya kufanya ziara katila baadhi
ya maeneo na kukuta hali hiyo na tayari ametoa agizo mchakato wa
kuwapatia fedha kaya zinazostahili uanze mara moja na kwa umakini mkubwa
na kuvitaka vyombo vya usalama kushirikiana nao ili haki iweze
kutendeka.
COMMENTS