Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bung...
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) David Kanyatta
akiwasilisha mada kwa Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na
Utalii kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi kunavyoathiri
sekta ya utalii katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma .
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Yussuf Hussein,
akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na wataalamu
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu utalii wa baharini ambao
umekuwa haupewi kipaumbele katika kutangazwa pamoja na kuendelezwa
katika semina hiyo.
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Marwa Chacha,
(katikati) akichangia hoja mara baada ya mada kuweza kuwasilishwa na
wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu wanyamapori
waharibifu wa mazao kama vile tembo wanavyoathiri maisha ya wapiga kura
wake kwenye vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika
semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Wengine ni wajumbe wa kamati hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Atashasta Nditiye,
(katikati) Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (
kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhandisi Ramo
Makani ( wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa makini michango ya wajumbe wa
kamati hiyo wakati walipokuwa wkichangia hoja kuhusu mada mbalimbali
zilizotolewa na wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu
madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo la ujangili wa tembo
na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama waharibifu wa mazao
kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi nchini,
iliyofanyika jana mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Devota Minja, MB ( wa
kwanza kulia) pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakifuatilia
kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wataalamu wa
Wizara hiyo kuhusu madhara ya kulishia mifugo ndani ya hifadhi, tatizo
la ujangili wa tembo na faru pamoja madhara yanayosababishwa na wanyama
waharibifu wa mazao kama vile tembo katika vijiji vinavyozunguka hifadhi
nchini katika semina iliyofanyika jana mjini Dodoma. Kwa upande wa
kushoto ni viongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj.Gen. Gaudence Milanzi (kulia) pamoja na na viongozi wa taasisi katika semina ya kamati
ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii iliyofanyika jana mjini Dodoma.
COMMENTS