VYUO VIKUU VYAAGIZWA KUTOTOZA ADA KWA FEDHA ZA KIGENI KWA WATANZANIA
HomeJamii

VYUO VIKUU VYAAGIZWA KUTOTOZA ADA KWA FEDHA ZA KIGENI KWA WATANZANIA

   Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma Vyuo Vikuu hapa Nchini vimeagizwa kuacha mara moja kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa w...

MAADHIMISHO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA YASISITIZA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU
WAKAMATWA KWA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA LA UMEME TANESCO YENYE THAMANI YA TSH 61,000,000
MKUU WA WILAYA YA HAI, BYAKANWA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KWA KUREJESHA SHAMBA LA FOFO ESTATE KWA HALMASHAURI YA WILAYA HIYO



 

 Na: Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma

Vyuo Vikuu hapa Nchini vimeagizwa kuacha mara moja kutoza ada kwa fedha za kigeni kwa wanafunzi ambao ni watanzania.

Agizo hilo limetolewa leo Bungeni, Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Jaku Hashimu Ayoub kwamba kumekuwa na malalamiko ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania ambao ni wazawa kulipishwa ada ya masomo yao kwa fedha za kigeni badala ya fedha za Kitanzania.

“Sarafu inayotakiwa kutumika Tanzania ni shilingi ya Kitanzania kwa mujibu wa kifungu cha 25 na 26 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT) ya mwaka 2006. Aidha, kwa Tanzania malipo ya kitu au huduma yoyote inapaswa kulipwa kwa shilingi ya Kitanzania kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha 28 cha Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania, 2006,” alifafanua Mhandisi Manyanya.

Aliendelea kwa kusema kuwa japo Wizara haijapokea malalamiko yoyote ya kutozwa fedha za kigeni kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu tangu itoe agizo kama hilo kwa wamiliki wa vyuo Septemba 07, 2016.

Hivyo basi kwa mara nyingine Mhandisi Manyanya ameviagiza vyuo ambavyo bado vinatoza wanafunzi Watanzania fedha za kigeni kuacha mara moja kwani vyuo hivyo vimeelekezwa kutoza wananchi wa Kitanzania kwa pesa ya Kitanzania.

Aidha Mhandisi Manyanya amewataka watanzania kutoa taarifa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa kuna Chuo chochote kinachotoza ada kwa Watanzania kwa fedha za Kigeni ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VYUO VIKUU VYAAGIZWA KUTOTOZA ADA KWA FEDHA ZA KIGENI KWA WATANZANIA
VYUO VIKUU VYAAGIZWA KUTOTOZA ADA KWA FEDHA ZA KIGENI KWA WATANZANIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFaP-7MvE6FSaf__f9B9x6Fa6WDHS7c4NGEmGHQFy14Bd0BT-jHYpNABty7DiRH47WoR-t0mT8rmJNAq4-vtt2mCyAfEahmqhxWusHUOEEZunXhrT-ZgB1RQKlbtohM9WrxxkhhMT-dwg/s320/Cl_IrNmWgAAAI4d.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgFaP-7MvE6FSaf__f9B9x6Fa6WDHS7c4NGEmGHQFy14Bd0BT-jHYpNABty7DiRH47WoR-t0mT8rmJNAq4-vtt2mCyAfEahmqhxWusHUOEEZunXhrT-ZgB1RQKlbtohM9WrxxkhhMT-dwg/s72-c/Cl_IrNmWgAAAI4d.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/vyuo-vikuu-vyaagizwa-kutotoza-ada-kwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/vyuo-vikuu-vyaagizwa-kutotoza-ada-kwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy