UNESCO YOUTH FORUM WAENDESHA SEMINA YA KUWAELEKEZA VIJANA NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI ZA UMOJA WA MATAIFA,CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO JIJINI DAR.
HomeJamii

UNESCO YOUTH FORUM WAENDESHA SEMINA YA KUWAELEKEZA VIJANA NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI ZA UMOJA WA MATAIFA,CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO JIJINI DAR.

Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali. ...

MWILI WA PROFESA BINAGI WAAGWA JIJINI DAR ES SALAAM KUELEKEA MKOANI MARA.
KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT YAIPIGA TAFU JUKWAA LA WAHARIRI MILIONI 1
VIDEO; PROFESA KITILA MKUMBO AZUNGUMZA BAADA YA KUAPISHWA NA RAIS MAGUFULI


Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali.
Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia  Global Peace Foundation (GPF) Tanzania
aliyewakilisha katika Semina hiyo Bi. Anna Mwalongo akielezea kwa kifupi
kuhusu Asasi hiyo.
Mshauri
wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi  Bw. Anthony Luvanda akitoa
masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea
kwa kufanya shughuli mbalimbali.
Baadhi ya vijana wakiendelea kusikiliza kwa makini mambo mbalimbali katika Semina Hiyo.
Bi.Bernice Fernandes akielezea namna alivyopata nafasi ya kwenda kusoma Marekani kupitia 'Scholarship'  na kuwasihi vijana wasikate tamaa kwa kuwa nafasi za kwendakusoma nje zipo nyingi.
 
Muandaaji wa Semina hiyo na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za
Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia.
Baadhi ya vijana wakiuliza maswali mbalimbali kwa wasemaji.
Picha ya pamoja ya watoa mada mbalimbali Kutoka Kushoto ni Frank Joash, Anthony Luvanda, Evance Exaud,Alice Norbert, Anna Mwalongo, Bernice Fernandes, Nelson Amar na Jackson Ogonga.
Watoa Mada wakiwa pamoja na Baadhi ya washiriki waliohudhuria Semina hiyo.

Picha na Fredy Njeje



Katika kuhakikisha vijana wanashiriki na kujikwamua katika mambo mbali mbali UNESCO  Youth Forum waliandaa semina ambayo ilihusu vijana kushiriki katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa, Kudumisha amani
kutoka ngazi ya vijana na jamii kwa ujumla ambapo Global Peace Foundation Tanzania walitoa mafunzo juu ya maswala hayo, kuhusu kusoma nje na kuelekezwa njia mbali mbali za kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi mbalimbali za kiraia.





Akizungumza na vijana hao kutoka vyuo mbalimbali na wale ambao walimaliza vyuo mwakilishi wa    asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Anna Mwalongo alisema kuwa Global Peace Foundation ni Taasisi
isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika, Ulaya, Asia na Marekani ni Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.” Alisema Anna.





Aliongeza kuwa Mnamo mwezi wa saba mwaka 2015 Global peace foundation waliandaa Mkutano mkubwa wa amani uliofanyinka Zanzibar uliojulikana kwa jina la Global peace Leadership Conference (GPLC Zanzibar) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais Mh. Balozi Seif
Ali na kuhudhuriwa na marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali. 

 "Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha kampeni ya “AMANI KWANZA” ambapo aliwalenga wanawake na vijana kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani, alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa GPF wanampango wa kupanua wigo zaidi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi kueleza mambo mbalimbali ya amani kupitia kampeni yao ya “VIJANA NA AMANI” " Alisema Anna





Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa
program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.





Nae Bi. Bernice Fernandes pamoja na Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili
‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.



Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na
kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao





Semina hiyo ilihudhuriwa na vijana kutoka vyuo vya, Chuo kikuu cha Dar es salaam, DUCE,TIA, NIT,Bagamoyo
University,DIT na TIA , wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine ambapo jumla yao walikuwa zaidi ya 196.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UNESCO YOUTH FORUM WAENDESHA SEMINA YA KUWAELEKEZA VIJANA NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI ZA UMOJA WA MATAIFA,CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO JIJINI DAR.
UNESCO YOUTH FORUM WAENDESHA SEMINA YA KUWAELEKEZA VIJANA NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA PROGRAMU MBALIMBALI ZA UMOJA WA MATAIFA,CHUO KIKUU CHA BAGAMOYO JIJINI DAR.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHsxat6eXnwRF-DdOT1uHANlzxVT7MsbsLZ9haJyHqIPHq7EqW09bcYD50UBfU2WlRdiaPc5y1cp5IeLW4aDIc41JK7oCP9JukXqr4qn0PzZWIruICd6L834dhhN5BxhYF2PoHtIn5qZ3a/s640/4.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjHsxat6eXnwRF-DdOT1uHANlzxVT7MsbsLZ9haJyHqIPHq7EqW09bcYD50UBfU2WlRdiaPc5y1cp5IeLW4aDIc41JK7oCP9JukXqr4qn0PzZWIruICd6L834dhhN5BxhYF2PoHtIn5qZ3a/s72-c/4.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/unesco-youth-forum-waendesha-semina-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/unesco-youth-forum-waendesha-semina-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy