Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani kufanya hi...
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa Dini
kuendelea kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani kufanya hivyo
kunaipunguzia serikali mzigo.
RC
Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina kwa Walimu
wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) na kusisitiza kuwa viongozi wa
dini wakiwafundisha mema waumini ambao ndiyo wananchi, Taifa halitakuwa
na wahalifu au matukio ya wizi, ujambazi, utumiaji wa dawa za kulevya na
ufanyaji wa biashara hiyo, jambo ambalo litaipunguzia gharama serikali
ya kuwahudumia waathirika kwa kuwapa vidonge vya Methadone, na serikali
haitatumia nguvu kubwa kujenga magereza kwa ajili ya wanaokiuka sheria
na taratibu za nchi.
Na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini kwani wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya Taifa hili.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa JUWAQUTA ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema kuwa lengo la semina hiyo ni
kuwaelimisha walimu hao juu ya kuunga mkono kauli mbiu ya HAPA KAZI TU
ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwani
kufanya kazi ni agizo kwa mujibu wa dini hiyo ya kiislamu ambapo waumini
wake wameambiwa wafanya kazi za halali ili wapate ridhiki halali na
siyo vinginevyo.
Huku
akifafanua kuwa hata manabii walikuwa wakifanya kazi hivyo ni vyema kama
viongozi kufuata nyayo hizio na kuwaamrisha wengine kufuata utaratibu
huo.
.Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi
semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar
es Salaam.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza katika
unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo
jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiombewa dua na viongozi dini,
leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Glob ya Jamii)
COMMENTS